Tumbusi, tumbusi kama wengi wanavyo mfahamu, huyu ni ndege jamii ya tai, au ndege wala mizoga. Hawa ni ndege wa kipekee sana na wapo aina zaidi ya 22 duniani kote, lakini kwa tafiti za hivi karibuni zimebaini na aina 15 tu. Katika mafunzo tuliyoyapata hivi karibuni kuhusu ndege hawa kwa undani wake, nimeona ni mafunzo na masomo ambayo mtanzania yeyote hapaswi kuyakosa kuyafahamu.