Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta.
Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi.
Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua.
Kampuni ya Radicati inakadiria kuwa takriban barua pepe bilioni 247 hutumwa kila siku. Inaelezwa kuwa asilimia 90 ya barua pepe hizo ni barua pepe hatarishi (SPAM) na Virusi, hivyo kuwa makini na barua pepe unazofungua.
Tweet ya kwanza ilichapishwa Machi 21, 2006 na Jack Dorsey
Nani alifahamu kuwa Twitter ingekuwa maarufu duniani kama ilivyo leo? Mnamo Machi 21, 2006 Jack Dorsey aliandika tweet ya kwanza iliyokuwa inasema, “Just setting up my twttr.” lakini hivi leo Twitter imeshakuwa na mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.
Video iliyotazamwa kuliko zote kwenye mtandao ni Despacito
Wimbo wa Despacito ulioimbwa na Luis Fonsi na Daddy Yankee ni wimbo unaoongoza kwa kutazamwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo huu umeshatazamwa mara bilioni 3.55 hadi sasa.
Saa 300 za video hupakiwa kila dakika kwenye YouTube
YouTube ni mtandao maarufu ambao wengi wanaufahamu kama mtandao wa kusambaza na kutazama video kwenye mtandao. Lakini je unajua kuwa kwa muda wa dakika moja video zenye jumla ya urefu wa saa 300 hupakiwa katika mtandao huu? Tovuti hii hupokea video kutoka kwa watumiaji mbalimbali duniani kote.
Neno kuperuzi mtandao (Surfing the internet) liliundwa mwaka 1992
Kabla ya mwaka 1992 neno (surfing the internet) halikuwa linafahamika hadi pale Jean Polly alipoandika makala iliyosomwa sana na kupakuliwa na watu wengi na kusababisha kusambaa kwa neno hili.
Mitandao ya kutafuta wapenzi inazalisha takriban dola bilioni 2.2 kila mwaka
Teknolojia imebadili mfumo wa maisha. Watu hutafuta wapenzi au wenzi wa maisha kwenye mtandao. Hili limepelekea tovuti za kutafuta wapenzi kuzalisha zaidi ya bilioni 2.2 kwa mwaka 2014 pekee.
China ina kambi za kutibu waathirika wa kutawaliwa na mtandao (internet addict)
Wakati china ikiwa na watumiaji wa intaneti wapatao zaidi ya milioni 721, inaaminika kati yao milioni 23 ni waathirika wa kutawaliwa na mtandao. Hivyo wameanzisha kambi mbalimbali za kuwasaidia watu hawa.
Watumiaji wengi wa intaneti ni roboti na programu haribifu (malware)
Wakati mwingine unaweza kufikiri watumiaji wa mtandao ni watu pekee. Lakini asilimia kubwa ni roboti na programu haribifu zilizobuniwa na watu mbalimbali ili kutimiza shughuli fulani.