Mbwa mwenye mnofu mdomoni hapigi kelele (Kifipa) Maana yake ni kama methali ya kiswahili isemayo:- Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Methali hii hutumiwa kwa kuwasema watu ambao wana kitu na huwasahau wale ambao hawana kitu. Zaidi, huweza kutumika kwa kuwaonya viongozi wanaosahau kuwatetea wenzao baada ya kupata madaraka na shibe.
Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha (Kikwere) Mwenda usiku hapa ni sawa na mtu ayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi. Lakini mwishowe jambo hilo lilipoonyesha mafanikio ndipo watu wakaanza kumsifu. Hutumika kwa mtu anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekeo hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.
Nguo ya mzee haikosi chawa (kimeru) Maana yake, mzee hakosi akiba. Maana ya methali hii itafahamika zaidi si kwa vile hali ya uchafu ndiyo iletayo chawa, bali kwamba kwa mzee huwa na akiba za aina aina nayo maana yake ni ile nzuri. Methali hii hutumika wakati mtu anapozungumzia utajiri wa mtu mzee. Ni kama njia ya kuwakoga wengine kwamba wakati wote utazamie kumkuta mzee katka hali nzuri, anayo akiba yake ambayo ameihifadhi.
Usidharau wakunga uzazi ungalipo (Kibena) Wakunga ni watu wenye kuheshimiwa sana kwa sababu ya ufundi na ujuzi wao wakati wa kuzalisha. Kwa kuchukua umuhimu wao huo, wanawake hushauriwa kutowadharau maadamu wangali wanazaa, isijeikawa wakti wa kujifungua wakakosa msaada. Matumizi ya methali hii ni kuwaonya watu kwa ujumla wasiwe na dharau kwa kitu ambacho kitawafaa katika maisha yao. Zaidi kwamba, kitu kilichokusaidi wakati uliopita usikidharau kwa vile hukitumii kwa wakati huu.
Hekima ni hali ya mtu anapopata ujuzi wa kudadisi, kuchanganua, kuelewa na kutenda au kusema kwa njia nzuri naya kukubalika na wengi. Maneno ya helima hutokana na tajiriba ya mtu, umri au ujuzi katika fani fulani, maisha, taaaluma, biashara au kazi.
Maneno mengine ya hekima yanakuwa katika semi za watu wa zamani wanaojulikana kama wahenga au wenye hekima wa zama za kale. Hapa pana baadhi ya maneno ya hekima yanayojulikana.
Maisha ni kile kinachokutatiza wakati unapangilia mikakati yako
Watu hujulikana maisha yao kwa masaibu yanayowapata na baadaye suluhisho ila si kwa wakati wao wa furaha.
Maisha ni asilimia kumi ya kile kinachonipata na asilimia tisini ni kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali
Wakati mwingi unaotumia maishani ni unapotafuta suluhu ya mambo yaliyokupata na muda mfupi ni ule ambao jambo mpya linafanyika maishani mwako.
Muda wako unakikomo, kamwe usipotee kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu mwingine
Ina maana kuwa unafaa kuishi maisha yako mwenyewe ila si kujaribu kuwa kama watu wengine kwani muda unaoishi duniani una mwisho.
Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotarajia
Ukiishi maisha yako ukifuata ndoto zako utaishi maisha ambayo utapendezwa nayo kwani mwishowe ndoto zako zitatimia ukitia bidii. Kama tujuavyo watu huangali mwisho wa safari bali si mwanzo wa safari.
Heshima ni kwa wale wasioupa mgongo ukweli, hata pale mambo yanapoonekana kufunikwa na giza na kutokufurahisha
Ni vyema kuishi maisha na ujasiri katika lolote unachofanya hata kama hujui matokeo yake kwani imani yako kwa jambo flani ndio hufanya jambo hilo kutendeka.
Kwa sababu kuwa huru si tu kutupa minyororo, bali kuishi katika namna inayoheshimu na kukuza uhuru wa wengine.
Hakikisha kuwa maisha yako na mienend yako inaonyesha kuwa uhuru wako una faida duniani