Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtu mwenye akili si yule anayejisikia kuogopa, bali yule aushindaye woga.
Woga hausaidii kwani woga hufanya mtu asifanye jambo ambalo huleta mafanikio baadaye kwa hivyo heri kuondoa woga maishani
 
Mara zote huonekana haliwezekani mpaka lifanikiwe.
Jambo huonekana kuwa ngumu kabla ulifanye lakini baada ya kulifanya watu hushangazwa na urahisi wa jambo hilo.
 
Ongoza kutokea nyuma -na wafanye wengine waamini wao ndio wako mbele.
Si vyema kujionyesha kuwa mwenye hekima kuliko wengine, heri kusikiliza wengine mara kwa mara
 
Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotarajia
Ukiishi maisha yako ukifuata ndoto zako utaishi maisha ambayo utapendezwa nayo kwani mwishowe ndoto zako zitatimia ukitia bidii. Kama tujuavyo watu huangali mwisho wa safari bali si mwanzo wa safari.
 
Maisha hayapimwi kwa idadi ya pumzi tuivutayo, hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu
Katika maisha yako jaribu kufanya mambo mengi yatakayo badili watu ili ukumbukwe kwani mambo ambayo unayafanya kumsaidia mwenzako ni yayo unazoacha duniani.
 
Kila wakati kabla ya kufikiria vitu ambavyo hauna chukua muda wa kuwaza vitu ambavyo unavyo
Ni vyema kuwa na mtazamo chanya maishani hivi basi usinugunike kwa vitu ambavyo hauna bali ushukuru Mola kwa vitu ambavyo amekupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…