Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wafungwa wanabakia kuwa watoto wa Mungu na wanahitaji kupewa thamani ya kiutu na kutendewa kiutu.
Ikumbukwe pia miongoni mwa wafungwa katika mazingira fulani haki haikutendeka. Hata kutoka maandiko ya dini mbalimbali tunasoma hayo.
 
Kutoka imani zetu na historia ya dini zetu tunaona kwamba wapo viongozi na wafuasi wa dini mbalimbali waliotumikia vifungo bila hatia yoyote. Pengine kwa kusingiziwa kutokana na kufundisha ukweli halisi wa maisha ya watu. Je twaweza kuthubutu kusema hawa walipoteza thamani yao mbele ya Mungu kwa kuingizwa gerezani?
 
Kwa wale waliongia gerezani kwa sababu ya uhalifu wa aina yoyote ile bado tukitafakari upendo wa Mungu kwa binadamu twaona, ni ule usio na mipaka. Yeye anawapenda wote maskini, wadhambi, dhaifu na wanyonge hata wakosaji na anawaita wote kuupokea mwaliko wa upendo wake, kujirudi na kuishi maisha yaliyo bora.
 
Haya si kutoka maandiko ya kidini tu bali hata yamewekwa katika Katiba za nchi na matamko mbalimbali ya kitaifa na kimataifa juu ya haki za Binadamu. Jitihada hizi zikilenga kuhimiza utekelezaji wake.
 
Raia wote tunaitwa na tunao wajibu wa pekee hapa kuonyesha huruma yetu kwa wale walio gerezani, na zaidi kufanya jitihada za pekee kusaidia wale ambao hawakutendewa haki waweze kurudishiwa iliyo haki yao.
 
Raia wote tunaitwa na tunao wajibu wa pekee hapa kuonyesha huruma yetu kwa wale walio gerezani, na zaidi kufanya jitihada za pekee kusaidia wale ambao hawakutendewa haki waweze kurudishiwa iliyo haki yao.
 
Kwa upande wa idara ya Magereza tunao wajibu mkubwa wa kuwatendea kiutu na kuwasaidia watoto wa Mungu walio gerezani kujiunda upya ili waweze kutoka gerezani wakiwa raia wema wanaoweza kutoa mchango wao katika kujenga Taifa letu.
 
Hata hivyo jamii inapaswa kutafuta sababu za watu kufanya vitendo vya uhalifu vinavyopelekea kuhukumiwa kwenda jela, na jamii hiyo hiyo kwa pamoja inao wajibu wa kutafuta njia ya kukabiliana na sababu hizo ili walau kuweza kuzipunguza kama sio kuziondoa kabisa. Mathalan matatizo ya umaskini, kukosa ajira, elimu duni, inafaa kwanza kupunguza matatizo hayo kama ikiwa kweli tunataka kupambana na uhalifu ndani ya jamii yetu.
 
Inafaa pia ieleweke kwamba kuweka watu gerezani na kuwatunza ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi, na wakati huo huo magereza yanaonekana sio njia madhubuti ya kupambana na uhalifu.
 
Utafiti uliofanyika katika nchi nyingi unaonyesha kuwa mbali ya kuongezeka wafungwa bado uhalifu uaendelea kuongezeka hivyo kuna haja ya kufikiri upya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…