Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la mgandamizo wa damu kuwa mkubwa na kwa lugha nyepesi ya mtaani watu huliita tatizo hili – blood pressure. Katika ukurasa wetu wa leo tumedhamiria kueleza nini maana ya mgandamizo wa damu kuwa mkubwa (high blood pressure),
 
dalili ambazo ukiziona ujue kuwa unanyemelewa na tatizo hili, namna ya kupima mgandamizo wa damu na tiba ambazo unaweza kutumia pale itakapobainika pasi shaka kuwa una tatizo hili la high blood pressure.
 
Kwanza tuwekane sawa kuwa msukumoo wa damu ni muhimu kwa maisha yetu, bila kuwepo na msukumo wa damu wa kuifanya damu izunguke ndani ya miili yetu, hewa ya oksijeni na virutubisho havingeweza kupita kwenye ateri na kuvifikia viungo vya miili yetu.
 
Kuna kipimo kinachotakiwa ili kuziwezesha
chembechembe za damu, zikiwemo chembechembe za damu nyeupe kwa ajili ya kinga, kuzunguka katika miili yetu.
 
Mgandamizo Wa Damu (Blood Pressure) Ni Nini?



Mgandamizo wa damu ni nguvu ya damu ya kusukuma kuta za mishipa ya damu. Nguvu hiyo inategemeana na uwingi wa damu inayosukumwa na moyo na uwezo wa mishipa ya damu ya arteri wa kuhimili nguvu hiyo.
 
Mgandamizo Wa Damu (Blood Pressure) Ni Nini?



Mgandamizo wa damu ni nguvu ya damu ya kusukuma kuta za mishipa ya damu. Nguvu hiyo inategemeana na uwingi wa damu inayosukumwa na moyo na uwezo wa mishipa ya damu ya arteri wa kuhimili nguvu hiyo.
 
Kiwango cha damu inayosukumwa na moyo kikiwa kikubwa na kipenyo cha arteri kikiwa kidogo, mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri hizo utakuwa mkubwa. Kadri uwingi wa damu utakavyoongezeka kutoka kwenye moyo au kipenyo cha arteri kitakavyopungua, ndivyo mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri utakavyoongezeka.
 
High blood pressure ni hali ya kuwepo kwa muda mrefu kwa mgandamizo wa damu kwenye kuta za arteri ambao ni mkubwa kiasi cha kuweza kuleta matatizo ya kiafya.
 
Unaweza kuwa na tatizo hili la kuwa na mgandamizo mkubwa wa damu – high blood pressure au hypertension – kwa miaka mingi bila kuanza kuona dalili zo zote au kutopata matatizo yo yote.
 
Pamoja na kuwa hujaanza kuona dalili zo zote, uharibifu wa mishipa ya damu na moyo huendelea na baadaye unaweza kupata matatizo makubwa ya kiafya kama shinikizo la damu (heart attack) na kiharusi (stroke). Yafaa basi kujipima na kujua mapema kuwa una tatizo la high blood pressure ili uanze kuidhibiti hali hiyo.
 
Tatizo la kuwa na mgandamizo mkubwa wa damu huongezeka taratibu kwa miaka mingi na karibu kila mmoja wetu huathiriwa na tatizo hili. Inakladiriwa kuwa ifikapo 2025, watu bilioni 1.56 katika dunia watakuwa wanaishi na tatizo hili. Bahati nzuri ni kuwa linaweza kugundulika kirahisi sana na kudhibitiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…