Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Osteogenesis Imperfecta: Huu ni ugonjwa wa kurithi ambapo mifupa ya mgonjwa huweza kuvunjika kiurahisi kabisa. Pamoja na kuwa na mifupa dhaifu mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri, kuwa na meno dhaifu na kupinda uti wa mgongo.
 
Bone Cancers: Kansa ya mifupa inaweza ni ya kuanzia ndani ya mifupa au ile iliyoanzia katika viungo vingine vya mwili na kusambaa hadi kwenye mifupa, kwa mfano, kansa ya mapafu, kansa ya maziwa au kansa ya prostate. Kuna aina nyingi za kansa ambazo huanzia ndani ya mifupa kama leukemia, osteosarcoma, Ewing sarcoma, malignant fibrous histiocytoma na chondrosarcoma.
 
Rickets: Huu ni ugonjwa wa watoto wadogo ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu na inayoweza kuvunjika kwa urahisi. ni ugonjwa ambao unaambatana na maumivu ya misuli. Chanzo cha ugonjwa huu ni ukosefu wa vitamini D kwa hiyo ni ugonjwa unaoweza kuzuilika kiurahisi.
 
Osteomyelitis: Osteomyelitis ni ugonjwa unaotokana na bacteria ambao hushambulia mifupa. Ni tatizo ambalo huweza kutokea ghafla au likawa la muda mrefu. Tiba ya ugonjwa huu ni kutumia antibiotics na kama hali ni mbaya sana ni kufanya upasuaji kuondoa kile kipande kilichoshambuliwa.
 
Maana Ya Mfadhaiko Wa Akili (Depression)



Kila mmoja wetu ameshapata kuwa na huzuni wakati fulani, ni kitu cha kawaida kinachotokea wakati umepotelewa na kitu, kutokana na mihangaiko ya maisha au kutokana na kudharauiliwa.
 
Huzuni ikizidi na ikienda kwa siku nyingi mfululizo (wiki mbili au zaidi) na ikiambatana na hali ya kujiona kuwa si wa thamani tena, kwamba ni mtu usiye na msaada wo wote – basi hii inaweza kuwa ni zaidi ya huzuni. Unaweza kuwa umepata tatizo la kiafya – mfadhaiko, ugonjwa ambao kwa bahati nzuri una tiba.
 
Mfadhaiko ni ugonjwa unasababisha mtu kuwa na huzuni kila wakati na kukosa hamu ya kufanya vitu au kutenda yale aliyopenda sana kufanya zamani. Mfadhaiko ni ugonjwa unaoathiri namna mtu anavyojisikia, anavyofikiri na tabia yake.
 
Chanzo halisi cha ugonjwa huu bado hakijafahamika. Wataalamu wanasema kuwa ni muunganiko wa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na urithi, mazingira ya maisha, mambo ambayo mtu amekutana nayo katika maisha na sababu za kisaikolojia.
 
Mtu anaweza kukutana na jambo moja tu kubwa na baya katika maisha yake kama kufiwa na mtu wa karibu, mahusiano mabaya ya ndoa ua kubakwa na akapata mfadhaiko.
 
Mtu mwenye mfadhaiko hupungukiwa na uwezo wake wa kutenda kazi kiasi kwamba yeye na walio karibu naye wote huathirika.
 
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa ya kulevya. Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wenye magonjwa ya moyo, waliopatwa na kiharusi, wenye kansa, kisukari, ugonjwa wa Parkinson’s na baadhi ya magonjwa mengine huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na mfadhaiko.
 
Mtu mwenye mfadhaiko pamoja na magonjwa hayo mengine huwa kwenye hali mabaya zaidi ya kiafya na hupata shida zaidi kuutibu ugonjwa huu.
 
Mtu mwenye mfadhaiko pamoja na magonjwa hayo mengine huwa kwenye hali mabaya zaidi ya kiafya na hupata shida zaidi kuutibu ugonjwa huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…