Hapa ndipo panadhihirisha malalamiko ya wadau ya muda mrefu kwamba kuruhusu wachezaji wengi wa kigeni ni kudumaza mpira wa wachezaji wazawa kwa sababu hawapewi nafasi.
Ukiangalia timu nne za juu utagundua kwamba kwa kuwa na wafadhili wengi wameweza kuwa na uwezo wa kuwasajili wachezaji waliowahitaji na wachezaji wao wana mazingira mazuri ya kujiandaa kimazoezi na kimashindano.
Hiki ni kiashiria kwamba makocha na viongozi wa timu hizo wanatakiwa waanze kuchukua hatua stahiki na kujitathimini kwa kina ili inapofikia kuanza mechi za theluthi ya pili wafanye vizuri zaidi.
Ukiangalia tofauri ya pointi kati ya timu ya kwanza na ile ya tano, tofauti baina yao in alama tano, kati ya timu ya sita hadi 10 na moja tofauti ya alama ni nne na kati ya timu ya 12 na 16, tofauti ya alama ni tatu.
Tofauti ndogo hiyo baina ya makundi hayo matatu ni kiashiria tosha kwamba hakuna timu hadi sasa mwenye uhakika wa kuwa kwenye nafasi aliyopo sasa theluthi ya pili itakapokuwa imekamilika (mechi 20).
Hii ni moja ya sababu ambayo wadau wanaona kwamba ligi ya mwaka huu (2017/2018) imekuwa ngumu kwa sababu ya matokeo ya mechi nyingi kuwa aidha sare au ushindi mwembamba.