Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maisha ya familia

Akizungumzia maisha ya familia, Aneth anasema watoto wao watatu wanafahamu kuhusu hali zao kiafya na baada ya kulitambua hilo, hawakupata mshtuko kwa sababu wamekuwa wakiishi kwa amani, hivyo wameendelea kuwa na amani.

Anasema kwa upande wa ndugu jamaa na marafiki, pia wanalitambua hilo baada ya mumewe kuchaguliwa kuwa kiongozi wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kitaifa.
 
Je alizipokeaje taarifa za mumewe kuathirika

Anasema taarifa za mume wake kuathirika hazikumshtua sana, “tulitoka Njombe mwaka 1995 kuhamia Morogoro, huko tumeishi kwa miaka sita wakati anaondoka kwenda Njombe tena, aliniacha nikiwa na mtoto wa mwezi mmoja na nusu, kwa hiyo tangu 1998 hadi 2000, alikuwa akiishi na yule mke mwenzangu na mimi nilirudi Njombe 2001 na mwaka huohuo, Yule mama alifaraiki dunia.”
 
Anasema aliwahi kupima afya yake mwaka 2003 kwa agizo la mchungaji, lakini hakupatikana na maambukizi, akapima tena mwaka 2008 ikaonekana hana, hivyo ameendelea kupima hadi mwezi wa tisa mwaka huu, bado damu yake inaonyesha hana maambukizi.

Mwanamke huyo anayejivunia kuwa mama bora wa familia yake anasema, yeye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Igelehedza na amekuwa akifanya kazi hiyo tangu 1987.
 
Mume wangu tangu awali ni mkulima na mfugaji, lakini kwa sasa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Taifa,” anasema Aneth.

Anasema licha ya mumewe kuathirika, bado wanazungumza namna ya kujilinda ili kuepusha maambukizi mapya.
 
Tumeambizana, huenda alipata maambukizi kutokana na mwenendo wake wa zamani lakini sasa inabidi abadilike, na sasa anamjua Mungu, inabidi tuishi maisha yanayompendeza. Maneno hayo yamemsaidia maana angekuwa nje ya imani huenda angeendeleza tabia ya awali.”

Je anatumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi?
 
Anasema mumewe baada ya kugundulika ana maambukizi, alinzishiwa dawa za kufubaza makali yaani (ARV).

Lakini pia kama mke, anajitahidi anampikia vyakula vizuri vinavyompatia lishe ya kutosha ili kumuepusha na maradhi nyemelezi.

Je! Mwinuka anawazungumziaje waathirika wengine?
 
Anasema licha ya changamoto anazokutana nazo, anawashukuru baadhi ya wanaume waliathirika kwa kuwa waelewa, hasa wale waishio vijijini.

Anasema anatambua wanaishi kwenye mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu, ufahamu na hali ya uchumi na wengine hukosa huduma za afya ingawa Serikali ina mtazamo wa kusogeza huduma katika ngazi za chini.
 
Anasema: “Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha maambukizi makubwa yapo kwa vijana wa miaka 15 hadi 24, sera hapo inasemaje kuhusu kuwanusuru vijana hawa? Inamzungumzia yule wa kuanzia miaka 18 na kuendelea sera imeongelea humo na hawa wengine sera haijawagusa lazima tubadilike, hawa wa miaka 15 hadi 17 wanasaidiwaje?”
 
Hali ya Ukimwi Tanzania

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) inasema, kundi linaloathirika na maambukizi mapya kwa sasa nchini ni la vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ambao ni sawa na asilimia 40 ya wanaopata maambukizi mapya kila mwaka, huku kati yao, asilimia 80 ni wasichana na 20 ni wavulana, hivyo kufanya katika kila vijana 10 wenye maambukizi, wanane ni wasichana na wawili ni wavulana.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko anasema hali ya maambukizi mapya ya VVU kwa sasa ni takribani watu 55,000 wanaambukizwa kwa mwaka, huku asilimia 40 wakiwa ni vijana.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega anasema ni wakati sasa wa kuwekeza katika matumizi ya kondomu kwa vijana wa rika hilo.

Ulega anasema mkakati huo unakusudia kuongeza matumizi ya kondomu kwa wanawake na wanaume kutoka asilimia 34 kwa wanawake na asilimia 40.5 kwa wanaume kwa takwimu za mwaka 2012, hivyo hadi kufikia 2018, Serikali inataka ifikie asilimia 55 ya matumizi ya kondomu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…