Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.
 
Dar es Salaam. Mgonjwa wa kwanza kupandikizwa figo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prisca Mwingira ameruhusiwa kurudi nyumbani leo Ijumaa baada ya kuwa chini ya uangalizi wa jopo la madaktari bingwa wa figo kwa siku 10.
 
Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa mara baada ya kutoka chumba cha uangalizi maalum (ICU), Prisca ameishukuru Serikali kugharamia matibabu yake na kuiomba kuwekeza zaidi katika matibabu ya kibingwa ili kusaidia Watanzania wengi wasio na uwezo wa kufuata gharama nje ya nchi.
 
Kwa kipekee napenda kumshukuru sana ndugu yangu, kaka yangu Batholomeo kwa kupenda niendelee kuishi. Madaktari bingwa wa figo Muhimbili tangu wamenipokea wamekuwa wakinipa matibabu mbalimbali, nimesafishwa damu kwa muda wa mwaka mmoja wamenishauri na mpaka katika matibabu ya kupandikiza figo nyingine,"
 
Nairobi, Kenya. Chuo Kikuu cha Nairobi kimefuta cheti cha shahada ya sheria ya Seneta wa Meru, Mithika Linturi kwa tuhuma za kutumia stakabadhi bandia kusajiliwa katika chuo hicho.
 
Uamuzi huo uliafikiwa na Baraza Kuu la chuo hicho baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa ushirikiano na Tume ya Elimu ya Juu kuhusu uhalali wa stakabadhi alizotumia seneta huyo kusomea sheria katika chuo hicho.
 
Hata hivyo, seneta huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa uamuzi wa chuo hicho umechochewa kisiasa na kwamba alitumia vilelezo sahihi kusajiliwa chuoni hapo.
 
Hii si mara ya kwanza kwa Linturi kupata pigo kuhusu elimu yake kwani wiki moja iliyopita Jaji wa Mahakama ya Juu mjini Meru, Ann Ong’injo aliagiza tume ya uchaguzi pamoja na ofisa aliyesimamia uchaguzi eneo hilo, Samuel Gichichi kuwasilisha nakala za vyeti halali vya elimu vya seneta huyo. Hatua hiyo ilikuja baada ya Mugambi Imanyara kupinga kortini ushindi wa Linturi kama Seneta wa Meru.
 
Linturi alikuwa miongoni mwa wanasiasa 106 waliokuwa wanachunguzwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC)kwa madai ya kikiuka kipengele cha maadili katika katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.
 
Dar es Salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amepewa kazi ya kubomoa jengo la Tanesco Ubungo, leo Ijumaa ameanza kusimamia shirika hilo litoe madirisha, vitu pamoja na viyoyozi ili waanze kazi ya kubomoa kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli.
 
TBA imechelewa kuanza ubomoaji wa jengo hilo baada ya Tanesco kuomba waondoe wenyewe madirisha, milango na AC, kazi ambayo amepewa kuifanya mpaka leo Ijumaa jioni kabla ya ubomoaji kuanza.
 
Akizungumza na gazeti hili leo Ijumaa wakati uondoaji wa madirisha ukiendelea, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga amesema kazi waliyonayo ni kubwa lakini wamejipanga kuikamilisha kwa wakati.
 
Mpaka sasa hatujapata mchoro wa jengo hili baada ya kujengwa, tunachofanya ni kupima na kuchora ili kuepusha madhara. Unaweza ukakata bomba la gesi hapa ikawa shida tena," amesema Mwakalinga.
 
Amesema suala kubwa wanalolizingatia kwenye ubomoaji huo ni usalama na kwamba watatoa mafunzo maalumu kwa wafanyakazi kuhusu kujikinga wakati kazi hiyo ikiendelea.

Amebainisha kwamba watabomoa jengo la mbele pekee bila kuathiri lile la nyuma. Hata hivyo, amekiri kwamba jengo litakalobaki litakosa mwonekano mzuri kwa sababu sehemu ya mbele inayobeba sura ya jengo itakuwa imeondolewa.

"Tutatumia teknolojia mbili katika kubomoa jengo hili ambazo ni manual na mechanical. Tungeweza kutumia njia ya kulipua lakini tumeona itaathiri shughuli nyingine za kiuchumi," amesema.
 
Mwakalinga amesema athari zitakazojitokeza wakati wa ubomoaji ni kelele pamoja na vumbi. Amesema wamefanya tathmini ya jengo na kuangalia athari za mazingira na kujiridhisha kwamba ni chache.

Kuhusu gharama za ubomoaji, Mwakalinga amebainisha kwamba bado hawajakubaliana kuhusu hilo lakini watakaa na Tanesco kuzungumza kuhusu gharama hizo.
 
Sheria ya manunuzi ya umma inasema ukishampa mtu kazi bila kutangaza tenda mnapata fursa ya kukaa na kujadili gharama wakati kazi inaendelea. Kwa hiyo, tutakaa na kuzungumzia hilo, hii ni taasisi ya umma na agizo limetoka kwa Rais," amesema Mwakalinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…