Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rais John Magufuli alishangaza wengi alipotaja jina la mfungwa aitwaye Mganga Matonya, mwenye umri wa miaka 85, wakati akitangaza msamaha kwa watu 61 waliohukumiwa kunyongwa na mmoja aliyekuwa na kifungo cha maisha.
 
Haikuwa kitu cha kawaida kwa mkuu wa nchi kutaja jina la mfungwa, lakini ni mwendelezo wa maajabu yaliyowahi kumkuta Matonya katika maisha yake ya gerezani. Mara ya kwanza alifutiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere.
 
Namshukuru sana Rais Magufuli,” alisema Matonya alipoongea na mwandishi wetu jana akiwa kijijini kwake Wiliko mkoani Dodoma.
 
Sikutegemea kama nitatoka gerezani. Naomba salamu zimfikie kwani sijui namna ya kuonana naye. Ningebahatika kuonana naye siku ile nilipotoka gerezani, ningemkumbatia kwa furaha.”
 
Matonya alipata taarifa za msamaha akiwa gereza la Kingolwira mkoani Morogoro, lakini awali alikuwa Gereza la Isanga mkoani Dodoma akiwa mahabusu baada ya kufanya kosa akiwa na umri wa miaka 39. Aliishi Isanga hadi Mei 10, 1980 wakati alipohukumiwa.
 
Hakimu aliamuru ninyongwe mpaka kufa. Wakati nasubiri utekelezaji wa hatua hiyo mwaka 1984, rais wa wakati huo, Julius Nyerere alinibadilishia adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha maisha,” alisema Matonya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…