Tuliandaa mpango wa kujiongezea mifugo. Baada ya kujiridhisha wapi tunaenda kuiba mifugo hiyo, tuliamua kwenda,” alisema Matonya.
“Haikuwa mara yetu ya kwanza. tulishafanya matukio kama hayo maeneo mengine. Lakini, kwa hili, arobaini za mwizi zilikuwa zimefika. Tulipata upinzani mkubwa uliosababisha mapigano na kifo cha mwenye mali.