Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ulipokuwa sekondary akaja mtu wa chuo akamchukua mpenzi wako, ukaenda chuo akaja mtu anayefanya kazi akamchukua mpenzi wako, ukapata kazi akaja mwenye gari lake akamchukua mpenz wako, ukanunua gari akaja mtu aliyeoa akamchukua mpenzi wako, ukaamua uoe kinakuja kiben10 cha chuo kinamchukua mke wako
 
Ubongo wa binadamu ni kiungo cha ajabu sana. Unafanya kazi masaa 24, siku 7 za wiki toka siku unazaliwa. Unaacha kufanya kazi siku ukiwa kwenye mtihani
 
1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito.
 
2. Samaki kutoa baharini, asa wenye magamba ambao huwa na virutubisho vya zinc vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu za kiume.
Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kuku huwa na kiasi kikubwa cha madini haya.
 
3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia kuondoa mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya moyo.
 
4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia.
 
5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo husaidia kujenga misuli imara. Pia ina bacteria rafiki wanaosaidia kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo.
 
7. Nafaka, vyakula hivi huongeza nguvu na huwa na nyuzinyuzi kusaidia kupata choo vizuri na kuimarisha mwili wako.
 
9. Mboga za majani na matunda, kama pilipili, machungwa, karoti, spinachi na maboga zina kemikali na virutubisho vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili, kuzuia kuzeeka mapema na kukukinga na saratani.
 
TOFAUTI na vyakula vingine, ndizi zinafaida kubwa sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.
 
Ndizi zina faida zipi katika urembo?
Chanzo cha nishati Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati kubwa, sukari iliyomo katika ndizi ni chanzo kizuri sana cha nishati.
 
Hivyo naweza kusema kuwa ndizi ikiliwa ipasavyo itakusaidia kujenga mwili na misuli yako kwa ujumla. Husaidia kuondoa chunusi Chunusi ni miongoni mwa matatizo ambayo huwasumbua warembo wengi hususan wanawake.
 
Je, unafahamu kuwa ndizi mbivu zinaweza kukuondolea tatizo hilo? Kwa kuchanganya ndizi mbivu na maziwa na asali na kisha kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.
 
Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…