6.Sauti ya mkwaruzo au kikohozi kikavu cha zaidi ya wiki mbili Hata hivyo ifahamike kuwa dalili hizi zinaweza kutokea pia kwa baadhi ya magonjwa mengine tofauti na saratani ya koo
Hivyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi. UCHUNGUZI NA VIPIMO Vipimo kwa ajili ya utambuzi wa saratani ya koo ni pamoja na Aina ya X ray iitwayo Barium swallow ambayo huonesha muundo wa koo pamoja na tumbo (stomach).
Kwa sasa, njia hii ndiyo ya uhakika zaidi ya kutambua uwepo wa seli za saratani katika koo. Iwapo itathibitika kuwepo kwa saratani katika koo, madaktari hupendelea kufahamu hatua ya ugonjwa ilipofikia. Kitendo hiki huitwa staging
Faida ya kufanya staging ni kuwa husaidia kufahamu ukubwa wa tatizo yaani ni kwa kiasi gani seli za koo zimeathiriwa, iwapo saratani imesambaa na kuathiri maeneo ya jirani na kama imesambaa ni viungo gani vilivyo athirika.