Daktari anayehusika na magonjwa ya koo katika Hospitali ya Muhimbili Theresia Uisso alisema kuwa ugonjwa wa mafindofindo unaweza kutibika kitaalamu tofauti na watu walio wengi kusema unaibika kwa kutumia chumvi.
Dalili kuu ya ugonjwa huu ni vidonda kooni. Mara nyingi mgonjwa hulalamika kuwa na vidonda kooni ambavyo huambatana na maumivu makali wakati wa kumeza chakula.
Dalili nyingine zinazoambatana na vidonda kooni ni uvimbe wa tezi unaodhihirika mbele ya shingo, homa kali, kichwa kuuma, mafua, harufu mbaya kinywani, kufifia au kupotea kwa sauti na mwili kuchoka, uchovu mkubwa na usingizi usioisha,koo kuuma(madonda kooni) hunaweza kudhani ni dalili za MALARIA
Mtu anaweza kupata Ugonjwa wa mafindofindo kutokana na kuongezaka kwa umbile la tezi ya pua ambapo kuna uhusiano mkubwa na maambukizi ya virusi na bacteria kooni hali ambayo upelekea mafindofindo kuongezeka ukubwa.
Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.
Pia ugonjwa huu husababishwa na upungufu wa cell nyeupe za damu katika mwili ambazo cell hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi (lymph) zinavimba na husababisha Tonsils.
Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata ugonjwa wa mafindofindo kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata (tonsils), mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.
Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto.
Kutokana na mtandao huu mkubwa wa celi za kinga mafindofindo huweza kutolewa bila kuathiri kinga za mwili ambapo hii imethibitishwa na tafiti mbalimbali na wadau wa afya duniani.
Pia ugonjwa huuunaweza kutibiwa kwa njia ya kufanyiwa upasuaji ambapo ni vema mafindofindo ya tolewe kwa njia hiyo.
Mtu anaweza kufanyiwa upasuaji kama anapata maambukizi ya kurudiarudia , yametunga jipu au ni makubwa kiasi cha kuathiri njia hewa au chakula.