3. Nyongo kubakia kwenye mfuko wa nyongo-unapomaliza kula chakula kwa kawaida nyongo yote hutoka na kwenda kusaidia katika umeng'enywaji wa chakula. Kama itatokea mfuko wa nyongo kuachia nyongo kidogo na nyingine kubakia kwa muda mrefu,basi tatizo la mawe ndani ya mfuko wa nyongo hutokea.
Tiba Ya Mgonjwa Mwenye Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo
Ili tiba ya mgonjwa mwenye gallstone iwe na ufanisi,ni lazima sababu zinazosababisha mawe kutokea. Kuepuka cholestrol nyingi kujikusanya kwenye mfuko wa nyongo na kuondoa bilirubin iliyogandamana kwenye mfuko wa nyongo husaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo hili
Matatizo yote yanayosababisha mawe kutokea husababishwa na matatizo ya ini. Matatizo ya ini kama vile ini kuharibika (liver cirrhosis),ini kuwa na mafuta (fatty liver),homa ya ini (hepatits B,C na D) huweza kusababisha mawe kutokea.