Mbali ya adhabu hiyo kwa Star Media, Kilaba pia alitangaza viwango vipya vya gharama za mwingiliano baina ya mitandao inayotoa huduma za mawasiliano ya simu nchini vitakavyoanza kutumika Januari Mosi baada ya vinavyotumika sasa kufikia kikomo Desemba 31.
Alisema kampuni za simu zimekuwa na kigugumizi kukubaliana kuhusu viwango hivyo na kuingia mikataba ya mwingiliano kwa sababu ya masilahi ya kibiashara hivyo TCRA ililazimika kuingilia kati na kuvipanga kwa kufuata utaratibu kama ilivyoainishwa katika sheria namba 12 ya kuanzishwa kwake mwaka 2003.
Gharama za mwingiliano zitakazotozwa kwa dakika na mwaka kwenye mabano ni Sh15.60 (Januari Mosi, 2018), Sh10.40 (2019), Sh5.20 (2020), Sh2.60 (2021) na Sh2.00 (2022).
Alisema viwango hivyo vimepungua kulinganisha na miaka mitano iliyopita ambayo gharama zake za mwingiliano zilizokuwa zikitozwa kwa dakika na mwaka wake kwenye mabano ilikuwa Sh34.92 (2013), Sh32.40 (2014), 30.58 (2015), Sh28.57 (2016) na Sh26.96 (2017).
Kupungua kwa gharama hizi kutawezesha na kuongeza ufanisi katika shughuli za sekta zingine kiuchumi na kijamii, pia kutaongeza mapato ya watoa huduma na Serikali kutokana na ongezeko la matumizi ya huduma za mawasiliano,” alisema.
Alisema kwa sasa simu za mezani ni 127,976 na watumiaji wa simu za kiganjani imeongezeka kutoka laini 2,963,737 mwaka 2005 hadi kufikia laini 40,002,364, Septemba.
Alisema kwa sasa simu za mezani ni 127,976 na watumiaji wa simu za kiganjani imeongezeka kutoka laini 2,963,737 mwaka 2005 hadi kufikia laini 40,002,364, Septemba.