Tetenasi ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Wadudu hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhi, misumari au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk.
Tetenasi imegawanyika sehemu mbili.
1.Tetenasi inayotokea kwa watu wazima (adult) Tetenasi ya watoto (neonates)
Nani yupo hatarini kupata tetenasi? Kwa watu wazima (Adults)
Ikiwa umetobolewa na msumari una zaidi ya 32% kupata tetenasi.Ikiwa umeungua, au watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, au watu wanaojiwekea tattoo, watu wenye magonjwa ya meno, wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu
2.Kwa watoto.
Kama mama mjamzito hatapata chanjo ya tetenasi , au kujifungulia nyumbani, yupo kwenye hatari ya kumsababishia mtoto mchanga kupata tetenasi.