Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tukio hilo liliripotiwa polisi na majirani waliokuwa wakiishi karibu na waliouawa. Mauaji hayo yalifanywa Januari 4, Mtaa wa Matosa Darajani uliopo Kata ya Goba jijini Dar es Salaam.
 
Tayari Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limetangaza kumsaka Lekule. Jana, kaimu kamanda wa kanda hiyo, Benedict Kitalika alimueleza mwandishi wetu kuwa tukio hilo linatokana na wivu wa mapenzi.
 
Tayari Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limetangaza kumsaka Lekule. Jana, kaimu kamanda wa kanda hiyo, Benedict Kitalika alimueleza mwandishi wetu kuwa tukio hilo linatokana na wivu wa mapenzi.
 
Kitalika aliwataja kwa majina waliouawa kuwa ni Upendo, ambaye ni mke wa mhasibu huyo, mtoto wao wa miezi minne na Magreth Samwel ambaye ni shemeji yake.
 
Mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Hamidu Pondomo alisema siku ya tukio kaka wa marehemu alienda nyumbani kwa dada yake baada ya kutumwa na mama yake baada ya kushindwa kumpata kwa njia ya simu.
 
Mama wa marehemu alipoona Lekule amepiga simu na hazungumzi chochote, alipiga simu ya Upendo ikawa inaita bila majibu, ndipo alipoamua kumtuma mwanae wa kiume kwenda kumtazama dada yake,” alisema Pondomo.
 
Alisema baada ya kufika katika nyumba aliyokuwa akiishi, alikuta mlango umefungwa, alipokwenda dirishani alichungulia na kukuta miili mitatu ikiwa imetapakaa damu.
 
Baada ya hapo ndio taarifa zikatolewa polisi ambao walifika na kuvunja mlango. Walikuta mwili wa Magreth sebuleni ukiwa na jeraha kubwa kichwani, mwili wa Upendo na mtoto ukiwa chumbani, wao pia walikuwa na jeraha kichwani,” alisema na kuongeza,
 
Baada ya hapo ndio taarifa zikatolewa polisi ambao walifika na kuvunja mlango. Walikuta mwili wa Magreth sebuleni ukiwa na jeraha kubwa kichwani, mwili wa Upendo na mtoto ukiwa chumbani, wao pia walikuwa na jeraha kichwani,” alisema na kuongeza,
 
Leo (jana) tulimzika Pendo na mwanae. Magreth amesafirishwa kwenda Mara.”

Mmoja wa marafiki wa Pendo, Happiness Azaria alisema marehemu alikuwa na ugomvi na mumewe, hasa baada ya kuzaliwa kwa mtoto.
 
Waliishi miaka 10 bila mtoto ila nilimshauri marehemu aende kanisani kuombewa, na kweli alifanikiwa kupata ujauzito na kujifungua mwezi Oktoba. Ila tangu hapo ugomvi ndio ukaanza,” alisema Happiness.
 
Wakati uongozi wa kata ya Nyehunge wilayani Sengerema ukipitisha sheria ya kuwacharaza viboko 12 au faini ya Sh10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, Wilaya ya Tandahimba imekamata wanafunzi watano waliopata ujauzito mwaka jana.

Sheria hiyo ndogo imepitishwa juzi kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WODC) baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja uzito kuzidi kuwa sugu.
 
Ofisa mtendaji wa Kata ya Nyehunge, Mabula Enock alisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.

“Tumelazimika kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel Kipole aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wacharazwe viboko au kutozwa faini ya Sh10, 000 ama vyote kwa pamoja,” alisema Enock.
 
Agizo la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba mwaka 2017 wakati akikaribisha wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyehunge.

Mkazi wa kata hiyo, Mussa Kazimili alisema sheria hiyo ndogo itasaidia kupunguza tatizo hilo na kuwataka wananchi na wazazi kusaidia kubaini wanaume watakogundulika kufanya vitendo hivyo.

Diwani wa kata hiyo, Charles Mbogo alisema kitendo cha kukatiza masomo si cha kuungwa mkono, hivyo adhabu inapaswa kuongezwa na kuitaka jamii kuachana na suala hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…