Kuongeza hamu ya kula
Wakati mfumo wa homoni za oestrogen na progesterone unapobadilishwa kwa kutumia vidonge humfanya mtumiaji kuwa na njaa sana na hivyo kukufanya ule sana hali inayoweza kupelekea kuongezeka uzito. Lakini hakuna ushahidi madhubuti unaoonyesha uhusiano wa moja kwa moja kuwa dawa hizo zenyewe huongeza uzito.

Kubadilika kwa hisia (moody)
Wanawake ambao hukumbwa na matatizo ya kubalika kwa hali/hisia zao kama kuwa na hasira, kutotaka kusemeshwa, hali hiyo huongezeka pale anapotumia vidonge vya kupanga uzazi. Wanawake wa aina hii wanashauriwa kujadiliana na wenza wao kabla ya kuanza kutumia dawa hizi.
Wanawake wenye matatizo haya ya damu kuwa mabonge wanashauriwa kutotumia dawa hizi kwani zitawasababishia madhara zaidi. Lakini pia kabla hujaanza kutumia dawa, unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya.
Maziwa kuongezeka ukubwa
Vidonge hivi vinaweza kukusababishia maziwa yako kuongezeka ukubwa au kupata maumivu ya maziwa madhara ambayo yataanza kutoonekana baada ya kutumia dawa hizi kwa wiki kadhaa.
Kutokwa na uchafu ukeni
Baadhi ya wanawake hukumbwa na tatizo la mabadiliko ya utoaji uchafu ukeni hali ambayo huathiri kujamiiana kwao kutokana na kupungua au kuongezeka kwa muda na kiasi cha utoaji uchafu. Utoaji wa uchafu kwa njia ya uke si tatizo kwa wanawake, lakini kama utahisi kuna hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda hospitali.
Athari hizo za vidonge tulizozitaja hap juu sio zote ni mbaya. Madhara mengine kubwa za kutumia vidonge hivyo ni pamoja na kuumwa sana na kichwa, Maumivu ya nyonga, maumivu ya kifua, uono hafifu pamoja na maumivu ya miguu au mapaja.