2. Nataka/naomba ‘x’
Sisi sote ni wabinafsi. Kila mmoja anataka mafanikio, furaha, pesa nyingi, uhuru na muda, mapenzi, afya nzuri — na kila kilicho kizuri maishani, tunakitaka. Kutaka yote haya si vibaya na haiepukiki, lakini kudhani kwamba yanatakiwa yashushwe kwako na wewe uanze kufaidi itakusababishia msongo wa mawazo hasa pale utapoyakosa.