VITU GANI VINAWEZA KUPEKULIWA.
Mtu kama mtu anaweza kupekuliwa, kwa maana nguoni mwake kama mifukoni nk. Pia vifaa kama gari, ,meli, nk navyo vyaweza kupekuliwa. Halikadhalika nyumba kama nyumba nayo yaweza kupekuliwa pamoja navyo vifaa vingine.
JE WAWEZA KUPEKULIWA MDA WOWOTE.
Hapana, si kweli kuwa waweza kupekuliwa mda wowote anaotaka askari. Sheria niliyotaja hapo juu inasema mda wa kupekua ni kuanzia jua linapochomoza na mwisho ni linapozama.
Yametumika maneno jua kuchomoza na kuzama badala ya kutaja mda labda saa 11 za asubuhi mpaka saa 12 za jioni kwasababu ya utofauti wa jiografia ya sehemu na sehemu.
Muonekano wa saa 12 za jioni wa kanda ya ziwa ni tofauti na ule wa pwani nk. Kwahiyo kutaja saa kwa lengo la kumaanisha usiku unapoingia na unapotoka ingekuwa kama inapotosha.
MPEKUAJI KUAMBATANA NA SHAHIDI MWENYEJI.
Askari anayepekua aje na shahidi mwenyeji. Mjumbe au kiongozi kutoka serikali za mitaa ni mtu muhimu kuwa mwenyeji. Jirani pia anaweza kuwapo.
ORODHA YA VITU VINAVYOCHUKULIWA.
Ni lazima kila kinachochukuliwa kuandikwa kwenye orodha maalum . Orodha hiyo utaisaini wewe uliyepekuliwa, askari aliyekupekua, pamoja na mashahidi ambao ni mjumbe au serikali za mitaa au jirani mwema.
Hii huepusha badae kuambiwa kuwa hata kitu fulani ambacho kinajenga kosa kuwa kilikutwa kwako. Lakini pia ni muhimu kwa ajili ya kurejesha mali zako baadae zikiwa zimetimia.