Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tende bora zaidi huwa na faida na faida nyingi za kitiba lakini bei yake ni ghali na tende ya hali ya chini na ya zamani kuvunwa bei yake ni rahisi ukilinganisha na tende mpya lakini faida yake kimatibabu ni ndogo zaidi.
 
watumiaji wa tende watumie tende yenye kiwango cha juu ili wapate faida ya kitiba. Pia ni changamoto kwa wafanya biashara wa tende watuletee na kutuuzia tende zenye ubora zaidi. Aidha wanunuzi nao wanunue tende zenye ubora wasijali ughali wa bei bali wajali ubora. Kauli yangu ni kwamba "Tende rahisi faida ndogo kitiba" na "Tende ghali faida kubwa kitiba".
 
Lengo hapa ni kuelimisha jamii wala sio kuharibu biashara ya mtu. Nawahimiza tutumie tende katika miezi yote na wala si mwezi wa Ramadhani tu, na wale wasiokuwa Waislamu nawafahamisha kuwa tende si chakula cha Waislamu pekee bali ni cha watu wote.
 
FAIDA ZA TENDE KITIBA:
1) KIFUA,MAFUA: Saga kiasi cha tende kwenye blenda pamoja na asali na samli safi ya ng'ombe kisha changanya ndani yake kijiko kimoja cha chakula cha unga wa Habbat saudaa na tangawizi.
MATUMIZI: Kula vijiko viwili vikubwa asubuhi na jioni.
 
2) KUTOPATA CHOO: Tengeneza juisi ya tende na maji au maziwa, kunywa glasi moja asubuhi na jioni.
 
3) KUIPA MISHIPA YA FAHAMU NGUVU NA KUIMARISHA KUMBUKUMBU: Kula tende mara kwa mara huongeza kumbukumbu na fahamu.
 
4) NI DAWA YA KUREJESHA HESHIMA NYUMBANI (MUJARRAB): Hutia kisu makali. Chukua tende robo kilo uondoe mbegu zake na saga ndani ya brenda pamoja na maziwa ya ng'ombe ongeza ndani yake kijiko kimoja cha unga wa uwatu na hulinjani ya unga.
MATUMIZI: Kunywa glasi moja asubuhi na jioni kila siku.
 
5) MWANAMKE ANAENYONYESHA: Kunywa kila siku asubuhi na jioni mchanganyiko wa tende, maziwa na uwatu
 
6)UKAVU AU KUKAUKA KWA MDOMO NA KOO: Kunywa juisi ya mchanganyiko wa tende na maji asubuhi na jioni, hulainisha mdomo na koo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…