Nyota huyo, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa goti, anatajwa na jarida la Forbes kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 49, ambazo ni zaidi ya Sh Bil 100 za Tanzania.
Diarra, ambaye alikuwa anawaniwa pia na Jose Mourinho wa Manchester United, anatua PSG kumsaidia majukumu Thiago Motta, mwenye umri wa miaka 35. Lakini pia, atakuwa msaidizi wa Adrien Rabiot katika idara ya kiungo.
Muumini huyo wa Dini ya Kiislamu aliwahi kutozwa faini ya Pauni milioni 6.8 (zaidi ya Sh bil. 21 za Tanzania) baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Lokomotiv Moscow. Aliikacha timu hiyo baada ya kukorofishana na kocha Leonid Kuchuk.
Uvivu na mafanikio ni vitu ambavyo haviwezi kwenda pamoja. Hakuna mtu mvivu aliyefanikiwa, na katika wengi wa walioshindwa, uvivu ni tabia ambayo wanayo.
Mafanikio yanakuhitaji ujitoe kuliko ilivyo kawaida. Yanakutaka uwe tayari kuweka juhudi kubwa zaidi ya unavyotaka kuweka. Unahitaji kuusukuma mwili wako hata pale unapohisi kuchoka.