tumia muda kujali vitu vyako kama viatu, mikoba,nguo hii itafanya hata kama nguo zako si za bei ghali, eg futa pochi la leather na mafuta ili kuondoa mikwaruzo, tumia tissue paper kuifadhi bags zako kabla ya kuziweka mahali
Hifadhi vitu vyako vizuri kama nguo chafu weka katika dustbin usitupe tupe hovyo na zilizo safi kunja au ning’iniza katika hanger hii itasaidia kufanya nguo zako kuwa na muonekano mzuri kila siku na kuto kupoteza upya wake
Badilisha muonekano wa nguo mfano koti lenye mikono mirefu fanya liwe na mikono mifupi, bana suruali pana, badilisha suruali kuwa pensi. Jaribu vitu vipya kila siku uta pata mionekano mipya kila siku
katika ma begi kitu cha kwanza kuchakaa ni mikanda na vile vyuma kuchakaa, kama the rest of the bag bado ina dai (kuonekana mpya) unacho takiwa kufanya ni kwenda kwa fundi viatu au fundi yoyote anaye weza kubadilisha hizo chuma na mikanda, ili kupata muonekano mpya & expensive
Kuna wakati una tamani kuvaa kiatu ukaonekana kiatu chako cha bei ghali, kuna wale wenzetu ana weza akanunu kiatu cha bei ghali lakini kila akikivaa kinaonekana cheap ndio maana mara nyingi utakuta mtu ana ulizwa umenunua bei ghali hivyo kwanini? mbona kipo kawaida sana una kuta una kaa unajiuliza kwanini? nakosea wapi? hizi ndizo sababu 8 viatu vyako vinaonekana cheap
Kawaida ni kwamba platform ina pokuwa ndefu ndivyo ambavyo viatu vina zidi kuonekana vya bei nafuu, viatu ambavyo havina platform vina onekana vizuri na smart
hata kama ni kizuri vipi usinunue kama hakikutoshi, ndio una weza kuweka makaratashi, shoe pads lakini kama hakikutoshi utakuwa huja poteza muda wako tu bali utapoteza na hela yako. Kutembea na makaratasi kwenye viatu nayo ina hitaji moyo
Embellishment ina weza kuwa tricky saa nyingine kama havija rembwa inavyo takiwa, makoro koro yanaweza kusababisha kiatu chako kikaonekana cheap tofauti na vile vilivyopo simple na classic
hii huwaga ni aibu, lol una wezaje kununua viatu na kuvivaa na huwezi kuvitembelea? hata kama vina million dollar look kama huwezi kutembelea kwetu vitakuwa cheap
kama una nunua kiatu hakikisha hakija kwaruzika yaani ngozi haija toka, hata kama una nunua mtumba nunua vile ambavyo ngozi yake bado ipo vizuri, kama kiatu kime isha ngozi usinunue tafadhali
kulikua na trend ya viatu vuenye ngozi ya plastick vina waka kama vimepakwa mafuta lakini kwa sasa ukivivaa utaonekana cheap jaribu kununua viatu vya ngozi hata kama ni ngozi feki ‘Suede leather”