Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
Kijana mpole (that's how she calls you), mbona unaondoka kwa huzuni namna hiyo? Did you want to be that special someone? Ulishafunguka au huwa unaumia kimya kimya tu?
 
Uhusiano kati ya kuota meno na kuharisha kwa mtoto


Hatua ya kuota meno kwa mtoto wakati mwingine huwa ngumu sana kwa mtoto mwenyewe na mzazi pia. Meno ya kwanza huanza kutokea kuanzia miezi mitano hadi miaka miwili japo kuna wanaowahi na kuchelewa zaidi ya hapo.
 
Dalili za mtoto kuota meno ni kama mtoto kuanza kung’ata fizi ,kupenda kuweka vitu mdomoni,kukosa usingizi,kukosa hamu ya kula, kulia sana na mate kujaa mdomoni.Kumekuwa na imani potofu kuwa meno ya mtoto yanapoota husababisha kuharisha kwa mtoto au joto la mwili kupanda lakini mpaka sasa hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha vitu hivi viwili.
 
Sasa kwanini wazazi wanaamini kuna uhusiano kati ya hivi vitu????

Mtoto anapoanza kuota meno huwa na tabia ya kuokota vitu ovyo na kuweka mdomoni ili kupunguza ile hali ya fizi kuwasha na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kula vijidudu vinavyosababisha kuharisha.
 
Pia ni katika umri huu ambapo mtoto huanza kula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama na hivyo kama chakula hakijaandaliwa katika mazingira ya usafi kinaweza kusababisha maambukizi ya vijidudu hivi vya kuharisha
 
Imani hii potofu imefanya magonjwa mengi ya mfumo wa chakula kupuuziwa na kushindwa kutibiwa kwasababu wazazi wengi wanaamini kwamba kuota kwa meno ndo kunasababisha kuhara kwa mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…