Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukishindwa Kuzingatia Mambo Haya Mawili Tu, Utakwama.

Kila mtu anapanda kwenye ngazi ya mafanikio yake. Kila mtu anakimbilia ngazi ya mafanikio yake, pasipo kujali ni kitu gani ambacho anakifanya, lakini kila mtu yupo kwenye ngazi ya kuelekea kwenye mafanikio yake kwa namna fulani hivi.
 
Lakini jambo mojawapo ambalo linaweza likafanya mtu badala ya kupanda ngazi yake ya mafanikio na hadi kuweza kufanikiwa, anajikuta anarudi nyuma hio yote ni kutokana na matumizi ya muda wake. Muda unaoutumia unautumia vipi.
 
Ni watu wengi sana ambao matumizi ya muda wao hayajakaa sawa. Mara nyingi sana watu hawa hawafanyi vitu vya kuwasaidia kulingana na muda wao walionao. Ni watu wa kufanya sana vitu vinavyowakwamisha na kuwarudisha nyuma kimafanikio.
 
Unatakiwa ujue namna ya kutumia muda wako vizuri sana ili uweze kupanda ngazi yako ya mafanikio kwa ufasaha na kuweza kufanikiwa. Kama utakuwa unatumia muda wako hivyo tu kila wakati ujue kabisa unajiangusha wewe kwa kurudi nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…