Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KILIMO BORA CHA KAROTI : Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao mizizi, kwa kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa, nyekundu, njano. Karoti za sasa zimetokeza kutokana na karoti pori, Daucus carota. Karoti hutumika sana kwaajili ya kuongeza radha kama kiungo kwenye mboga au kwenye kachumbari na pia zinafaida kubwa katika mwili kwa kukupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma hasa pale mtu atafunapo.
 
HALI YA HEWA NA UDONGO.

Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao.
 
UTAYARISHA WA SHAMBA

Karoti zinahitaji Shamba la Karoti lilimwe kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 kwenda chini ya ardhi. Mkulima anatakiwa kuandaa matuta yenye mwinuko wa kimo cha sentimita 28 – 40 kwenye shamba, na upana wa mita 1, pia mita 1.5 umbali wa tuta moja hadi lingine. Kwa maandalizi mazuri tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu za karoti yenye umbali wa sentimita 15- 20, mifereji minne kwa tuta.
 
MBEGU

Jinsi ya kujua mbegu nzuri zenye uwezo wa kukua bila wasiwasi. Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha. Zilizopoteza uwezo wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga, kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda/kusia.
 
UPANDAJI

Inahitajika uoteshe kwenye kitalu ndipo uhamishie shambani.

Weka mbegu katika chupa ya milimita 100 na toboa kidogo mfuniko, baada ya hapo Sia mbegu katika mifereji ya kupandia kwa kutikisa chupa yenye mbegu, ndipo, Funika mbegu kwa kutumia mboji au mchanga, ukimaliza Nyunyiza maji ya kutosha, Funika tuta na plastiki nyeusi, hatua nyingine Kandamiza plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo.
 
Mbegu huota baada ya siku 3-5 kutegemea na hali ya hewa. Inakupasa kukagua shamba mara tatu kwa siku. Baadaye Ondoa plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota. Usicheleweshe kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo katika plastiki. Hapo tayari kwa kupanda shambani.
 
MBOLEA

Weka mbolea aina za asili (samadi au mboji) mwanzoni, ila kama haukutumia mbolea ya samadi au mboji, weka mbolea ya S/A kilogramu 100 kwa hekta kama haukutumia mbolea za asili, kama ulitumia mbolea za asili basi weka kilogramu 50 kwa hekta. kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji
 
UPALILIAJI & UNYEVU

Ili kupata mavuno mengi palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu na nyasi kwa kung’olea kwa mkono, jembe na mangineyo, na kwenye udongo hakikisha kuna unyevu wa kutosha kama sio kipindi cha mvua inatakiwa umwagilie shamba lako kwa wiki mara mbili.
 
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU WA ZAO HILI



MAGONJWA ;

Madoajani (Leaf Spot):
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano.

Ugonjwa ukizidi majani hukauka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…