Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. Mtu anayehamisha mlima, anaanza na jiwe moja.
Hakuna kinachoshindikana kwenye maisha ikiwa wewe utaamua sasa kwamba ni nini unakitaka. Yawe ni matatizo ukitaka yaondoke yataondoka au uwe ni mradi fulani, ukitaka kuufanya utaufanya na utakupa matokeo.
 
Kwa hiyo hata wewe usizuiliwe na kitu chochote, anza kuhamisha jiwe moja moja kwa chochote kile unachokifanya na itafika utafanikiwa. Usitishike na ukubwa wa mlima ulionao, anza kuhamisha wewe jiwe moja moja na mafanikio utayaona.
 
Kwa hiyo hata wewe usizuiliwe na kitu chochote, anza kuhamisha jiwe moja moja kwa chochote kile unachokifanya na itafika utafanikiwa. Usitishike na ukubwa wa mlima ulionao, anza kuhamisha wewe jiwe moja moja na mafanikio utayaona.
 
2. Watu ndio muhimu, vitu vingine tunavipata tu.
Katika hekima hii ya maisha na mafanikio inatuonesha unaweza ukapoteza pesa ukaipata, unaweza ukapoteza kitu chochote kile na ukakipata, lakini si kupoteza mahusiano au watu wako wa karibu na wenye msaada.
 
Mahusiano bora ndio msingi mkubwa wa mafanikio yetu pia. Inapotokea ukawa ni mtu wa kupotezea watu na kuthamini vitu, hiyo kwako unakuwa unajiweka kwenye hatari. Unapaswa kukumbuka kwamba watu ni muhimu, vingine tunavipata tukiweka juhudi.
 
3. Maelezo marefu, mwisho huleta uongo.
Kila mmoja anapaswa kujua anatakiwa kuwa mtu wa kutokutoa maelezo marefu sana kwa kitu ambacho kinaeleweka. Inatakiwa kueleza kitu kwa ufasaha na ikaeleweka pale kinapotakiwa na watu wakalitambua hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…