Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kisetu alisema wanawake hukumbana na vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha ushiriki wao katika nafasi na fursa za kuongoza ambavyo vinaanzia kwenye mfumo dume hadi ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kufanyia kampeni nyakati za uchaguzi.
 
Vilevile alisema kuna mfumo kandamizi wa kisiasa unaowanyima wanawake haki ya uongozi na ushiriki kwenye shughuli za kidemokrasia.

“Kongamano hilo litakuwa na matukio tofauti ambayo yatahitimishwa na azimio la pamoja la wanawake juu ya utambuzi na kuandikwa kwa michango ya wanawake,” alisema Kisetu.
 
Maktaba ya Mkoa wa Mtwara imeanzisha programu mpya ya kuwasaidia wanafunzi wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK) kuhakikisha wanakuwa na uelewa mpana.

Mkutubi Msaidizi wa Maktaba ya Mkoa wa Mtwara, Fred Mpoma alisema juzi wakati wa uzinduzi wa kusoma kwa kutumia maktaba mtandao.
 
Mpoma alisema kuwa shule nyingi zina uhaba wa vitabu vya kuwafundishia wanafunzi na hivyo ujio wa maktaba mtandao katika maktaba hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya upungufu wa vitabu katika shule za msingi mkoani hapa.
 
Tumeona shule nyingi za hapa hazina uwezo wa kununua vitabu kutokana na bajeti zao kuwa ni ndogo lakini kio –kiti (maktaba mtandao) itawasaidia walimu kupata vitabu ambavyo wanavihitajika kufundishia,” alisema.
 
Dada wa aliyekuwa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan Kasailo ametaja sababu ya kifo chake.

Hassan alifariki ghafla siku ya Ijumaa, ambapo kifo chake kilithibitiswa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta.
 
Kabla ya kuthibitishwa, taarifa za kifo cha hakimu huyo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiambatana na taarifa ya mtu aliyetajwa kwa jina la Mng’oa kucha ikitishia maisha ya hakimu huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni akizungumzia kifo hicho na vitisho hivyo vya mtandaoni alisema hana taarifa za kifo cha hakimu huyo na hakuwahi kuripoti kuhusu kutishiwa maisha.
 
Akizungumza jana baada ya mazishi ya kaka yake kijijini kwao Kwamsisi wilayani hapa, dada wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rehema Kileo alisema kwamba ndugu yao alipoteza maisha baada ya kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu..

Dada huyo alisema familia yao haina taarifa zozote kuhusu utata wa kifo cha ndugu yao kuwa alipata vitisho, lakini wanachojua wao alifariki kwa ugonjwa.
 
Chanzo cha kifo cha kaka ni ugonjwa wa presha, ilishuka sana hadi kusababisha kifo chake na si vinginevyo labda kama kuna hilo mlilosikia nyie,” alisisitiza Rehema akipinga uvumi wowote kuhusishwa na kifo cha kaka yake.
 
Awali, ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ulionyesha kuandikwa Februari 17 ukiwa na kichwa cha habari, “Tuondoleeni mtu huyu hakimu Ilala kabla hatujachukua sheria mkononi.”

Ujumbe huo ulimtaja hakimu huyo kwa majina yake na kumtuhumu kutoa hukumu kandamizi na kwamba huu ndio mwezi wake wa mwisho.
 
Tumeripoti sehemu mbalimbali tumechoka sasa huu ndio mwezi wake wa mwisho, yeyote anayemjua salam hizi zimfikie...” inasomeka sehemu ya ujumbe huo. Hata hivyo, uvumi huo unapingwa na familia ikieleza kuwa ndugu yao alikuwa na shinikizo la damu na ndilo lililochukua uhai wake.
 
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Grorious Luoga alisema mbali na suala la mipaka ya kimataifa, wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mipaka baina ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wananchi wanaoizunguka kwa kuwa wamekuwa wakivamia na kujenga ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…