Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati upotevu huu kwa nchi za baridi ni mdogo, makadirio ya upotevu huo kwa nchi za tropiki ni mkubwa mno. Katika baadhi za nchi za Afrika kiasi cha asilimia 30 ya mavuno huharibika kila mwaka.
 
Hata hivyo juhudi nyingi zinafanyika duniani kote kuhakikisha kwamba uzalishaji na hifadhi ya nafaka (Mahindi, Mtama, Uwele, Shayiri, Ngano), na mazao aina ya mikunde (maharage, kunde, mbaazi, choroko) na mbegu za mafuta(soya, ufuta, alizeti) vinafanyika kwa ustadi mkubwa ili kuokoa mazao haya yasiharibiwe ghalani.
 
SABABU ZA KUHARIBIKA KWA MAZAO

Umbile: Kwa kawaida katika mzigo wa nafaka asilimia 60 ya nafasi huchukuliwa na nafaka na sehemu iliyobaki huwa ni nafasi baina ya nafaka hizo.
 
Nafaka zinapowekwa kwa wingi mahali pamoja zina uwezo wa kuruhusu hewa kupita pia zina mpitisho kidogo wa joto.
 
Pia ikumbukwe kwamba mbegu mbalimbali hutofautiana katika ubora wa kuhifadhiwa katika maghala, hii hutokana na tofauti katika aina ya viini vilivyomo katika mbegu hizo vilevile ulaini au ugumu wa maganda ya mbegu huchangia katika kuamua kiasi cha uharibifu.
 
Unyevu: Hii ndiyo sababu kubwa ya kuharibika kwa mazao katika hifadhi. Mazingira yenye unyevu mwingi hupendelewa sana na wadudu waharibifu kama mchwa au vijidudu kama bakteria na fangasi. Vilevile mazingira ya aina hii husababisha mabadiliko ya kikemikali ndani ya mbegu na hatimaye kusababisha kumea kwa mbegu zilizo ghalani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…