Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unyevu: Hii ndiyo sababu kubwa ya kuharibika kwa mazao katika hifadhi. Mazingira yenye unyevu mwingi hupendelewa sana na wadudu waharibifu kama mchwa au vijidudu kama bakteria na fangasi. Vilevile mazingira ya aina hii husababisha mabadiliko ya kikemikali ndani ya mbegu na hatimaye kusababisha kumea kwa mbegu zilizo ghalani.
 
Hali ya Joto/Baridi: Kuongezeka kwa joto huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika mazao ghalani. Joto la juu kati ya sentigredi 21 mpaka 43 huchochea kuwepo hali ya unyevunyevu ghalani na kusabisha mbegu nyingi kumea. Joto kali sana zaidi ya sentigredi 66 husababisha kiini cha mbegu kufa pia huharibu gluten kwenye nafaka kama ngano ambayo ni muhimu katika uokaji wa mikate na vitafunwa mbalimbali. (Gluten ni protini inayosababisha mnato).
 
Viumbe: Wadudu husababisha kuharibika kwa nafaka zikiwa ghalani. Wadudu hawa ni kama mchwa, panya, ndege na fangasi. Wadudu hawa wakiwa katika mzingira tofauti wa joto na unyevunyevu huweza kuzaliana na kukua haraka na hivyo kusabisha uharibifu mkubwa wa mazao ghalani.
 
FAIDA YA KUHIFADHI:

Uhakika wa upatikanaji wa chakula nyakati zote za mwaka.

Faida ya kuhifadhi mazao ya chakula ni kumhakikishia mkulima bei nzuri baada ya msimu wa mavuno kupita. Vilevile walaji huhakikishiwa upatikanaji wa chakula nyakati zote, na bei haiumizi sana wanunuzi.

Pia huwezesha upatikani wa mbegu bora na zifaazo kwa ajili ya uzalishaji kwa misimu inayofuata.
 
Ngoko: Ni aina mojawapo ya maghala, hujengwa kwa nguzo za miti na majani yaliyosukiwa kwa kamba katika nguzo hizi. Huwa na kimo cha mita 2 hadi 3 na urefu wa mita 5 au zaidi. Kwa Kawaida hujengwa karibu na makazi. Hutumika kuhifadhi mazao kama mtama na mahindi ambayo hayajamenywa maganda yake.
 
Makapu au mashimo: Haya huwa duara na umbo la mstatiri na hujengwa kwa kutumia vifaa asilia. Kuta zake huwa za majani zilizoimarishwa na fito za mianzi. Hutumika kuhifadhi nafaka za aina mbalimbali.
 
Maghala ya kisasa: Haya ni kama yalivyo maghala asilia isipokuwa hujengwa kwa kutumia vifaa vya kisasa, Mfano:
 
Maghala makubwa: Mara nyingi hutumiwa na wakulima wakubwa, na kawaida hujengwa katika miji mikubwa ambapo mahitaji ya chakula yanazidi uzalishaji wa ndani ya nchi na usafirishaji wake kwenda sehemu za mbali ni rahisi. Maghala haya yana uwezo wa kuhifadhi kiasi kikubwa cha chakula kwa ajili ya matumizi ya dharura.
 
USALAMA KATIKA KUHIFADHI

Mipangilio mibovu na kutozingatia taratibu stahiki za kuhifadhi mazao, hupelekea kujenga mazingira ya kuzaliana kwa wanyama waharibifu na uvundo wa kuharibu nafaka zilizohifadhiwa.
 
Kanuni zifuatazo ni muhimu kuzingatiwa:

Ghala lazima lijengwe kwa ustadi mkubwa kusudi lifanye kazi iliyotarajiwa.

Ghala lazima likaguliwe mara kwa mara.

Mbegu zinazokubaliwa kuhifadhiwa lazima ziwe kavu, unyevu wake usizidi asilimia 12.

Usichanganye aina mbili au zaidi katika ghala.

Kila zao liwe na hifadhi yake.

Ghala lazima liwe na takwimu zionyeshazo kiasi cha unyevu, uzito, idadi ya magunia, muda wa hifadhi na kiasi kilichopo.

Tumia viuatilifu vinavyoshauriwa kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa mazao.

Magunia yasiwekwe kwenye sakafu, bali yawekwe katika machaga ili kuepuka kupata unyevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…