Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jina la Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho limerudi katika anga za uvumi kuwa kocha huyo Mreno anatakiwa na wababe hao wa Ufaransa endapo ataharibiwa na Manchester United katika pambano la nusu fainali FA dhidi ya Tottenham.
 
PSG itaachana na Emery baada ya kuchapwa katika mechi zote mbili dhidi ya Real Madrid hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na licha ya jina la Mourinho kurudi tena katika anga hizo, vita bado ni nzito katika kuwania kiti hicho.
 
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte naye anapewa nafasi ya kuchukua kiti hicho baada ya kubainika Chelsea itaachana naye mwishoni mwa msimu huu kutokana na kuwa na msimu mbovu licha ya ubingwa alioipa msimu uliopita.
 
Makocha wengine wawili mahiri ambao hawana kazi, Muitaliano Carlo Ancelotti na Mjerumani, Thomas Tuchel nao wamekuwa wakitajwa katika kuchukua nafasi hiyo lakini kurudi kwa jina la Mourinho katika anga hizo kumeamsha hisia za mashabiki.
 
Awali Mourinho alikaribia kutua katika klabu hiyo ya Paris mwaka 2016 wakati ilipomfukuza kocha wake wa zamani, Laurent Blanc lakini mwenyewe akatulia akisubiri nafasi ya kuifundisha Manchester United na klabu hiyo ikaamua kumchukua Emery ambaye alipata mafanikio na Sevilla kwa kuipa ubingwa wa Europa misimu mitatu mfululizo.
 
Emery katika msimu wake wa kwanza alipambana na Monaco na kushindwa kuipa timu hiyo taji la Ufaransa lakini klabu hiyo iliamua kusonga naye mbele huku ikimuongezea nguvu zaidi kwa kumnunua staa wa kimataifa wa Brazil, Neymar kwa dau la Pauni 198 milioni na kuvunja rekodi ya uhamisho ya dunia.
 
Hata hivyo, msimu huu wa pili bado ameshindwa kuonyesha makali yake katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kutolewa na Madrid katika hatua ya mtoano huku matajiri wa timu hiyo wakijiwekea malengo ya kutwaa ubingwa wa Ulaya zaidi.
 
Kwa upande wa Mourinho, kocha huyu wa zamani wa Porto, Inter Milan na Real Madrid anatazamiwa kukaa zaidi ya msimu huu lakini upepo unaweza kubadilika muda wowote Old Trafford endapo timu hiyo itachapwa na Tottenham katika pambano la FA hatua ya nusu fainali.
 
Taji hilo ni mafanikio pekee ambayo kocha huyo anaweza kuipa United msimu huu na kama itashindikana lolote linaweza kutokea baada ya kocha huyo kutumia zaidi ya Pauni 350 milioni kununua wachezaji mbalimbali lakini aina yake ya soka imeshindwa kukidhi matarajio ya mashabiki na mabosi wa United.
 
Kocha huyo pia amekuwa akiingia katika malumbano ya mara kwa mara na mastaa wake kama, Paul Pogba na Luke Shaw na wengineo na hivyo kuiweka timu katika presha isiyohitajika na kuna habari kwamba tayari baadhi ya wachezaji mastaa hawapo upande wake kwa sasa.
 
Juzi wakati wa maandalizi ya pambano dhidi ya Swansea wikiendi hii imeripotiwa kuwa aliitisha mkutano na wachezaji wakubwa klabuni hapo kwa ajili ya kusafisha hali ya hewa na kuokoa msimu huu ambao umeenda kombo huku watani zao Manchester City wakielekea kuchukua ubingwa wa England na wakiwa wanapiga hatua katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…