Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye orodha hiyo, Sanchez analipwa Pauni 450,000 kwa wiki huko Manchester United, akifuatiwa na Ozil, anayelipwa Pauni 350,000 kwa wiki. Kama Hazard atakubali ofa hiyo mpya, atakuwa namba tatu, Pauni 305,000 kwa wiki, si haba. Wengine wanaolipwa mishahara ya kibosi ni Paul Pogba (Pauni 290,000) kwa wiki huko Man United, wakati Kevin De Bruyne analipwa Pauni 280,000 kwenye kikosi cha Manchester City na anayekamilisha orodha hiyo ni straika Romelu Lukaku, anayelipwa Pauni 250,000 kwa wiki huko Old Trafford.
 
Shughuli pevu itakuwa huko Etihad. Kuna mmoja anataka kushinda abebe ubingwa, mwingine atagoma kugeuzwa ngazi, basi ni moto juu ya moto. Manchester City watakaokuwa wenyeji, watahitaji kushinda ili kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, lakini Manchester United wamejipanga kukataa kuwa ngazi ya ubingwa kwa mahasimu wao hao, wanaowaita majirani wapiga kelele.
 
Derby nyingine itakuwa ya heshima huko Merseyside, wakati Everton itakapoikaribisha Liverpool iliyokuwa kwenye ubora wake kwa sasa. Mechi hiyo ni ya kulinda heshima tu, huku Liverpool wakitaka fursa ya kutengeza mazingira mazuri ya kumaliza msimu ndani ya Top Four kwenye ligi hiyo.
 
Lakini, nahodha wa Man City, Vincent Kompany, amewaambia Man United wasifikirie watakuwa wamechanganyikiwa baada ya kufungwa 3-0 na Liverpool, kwani Ligi Kuu ni kitu tofauti na wao wanahamu ya kutangaza ubingwa mapema. Matokeo ya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya yanadaiwa yataichongea Man United na kuwafanya Man City wawe na njaa zaidi katika mechi hiyo.
 
Huko Liverpool, Kocha Klopp anaweza kumkosa staa wake Mohamed Salah, ili kumpa mapumziko awe fiti kucheza na Man City Jumanne ijayo. Man United wanamtegemea fowadi wao, Romelu Lukaku, ambaye amekuwa moto kwa siku za karibuni kwenye ligi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…