Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwananchi imechambua maswali na hoja hizo na kuziweka katika vipengele kumi na baadaye kuhoji wadau na pia kuchukua maoni ya watu waliojitokeza hadharani, kama bungeni na kwenye akaunti za mitandao ya kijamii, kuzungumzia suala hilo.
 
Maswali hayo yanajikita katika mila na utamaduni wa Kitanzania, sheria kama ya mtoto na ndoa, uwezekano wa mpango huo kutoa suluhisho, utayari wa watuhumiwa kuitikia wito, athari dhidi ya watoto, hadhi ya wahusika na mgongano unaoweza kutokea baina ya taasisi zilizopewa dhamana ya kushughulikia masuala hayo.
 
Maswali hayo yanajikita katika mila na utamaduni wa Kitanzania, sheria kama ya mtoto na ndoa, uwezekano wa mpango huo kutoa suluhisho, utayari wa watuhumiwa kuitikia wito, athari dhidi ya watoto, hadhi ya wahusika na mgongano unaoweza kutokea baina ya taasisi zilizopewa dhamana ya kushughulikia masuala hayo.
 
Ushauri wangu kama wizara inayosimamia haki za watoto, suala hili linapaswa kufanyika kwa faragha kwa sababu una-deal na watu,” alisema Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile, ambaye wizara yake pia inaongoza Idara ya Ustawi wa Jamii.
 
Anachokifanya RC Makonda ni jambo zuri, lakini linahitaji uangalifu na tufuate mifumo sahihi. Nitoe wito kwa wananchi wote kufuata taasisi zinazohusika.”

Dk Ndugulile ni mmoja wa watu waliozungumzia suala hilo, wakijibu moja ya maswali yaliyoibuka kuhusu utaratibu wa kushughulikia masuala ya malezi na ndoa, ambayo hushughulikiwa na taasisi zinazohusika kwa njia ya faragha
 
Kauli yake inatokana na hali iliyojitokeza kwenye ofisi hiyo, ambako wanawake wengi walienda wakiwa wamebeba watoto na kuachia baadhi ya watu kuwapiga picha na baadaye kuzisambaza mitandaoni, ikiwemo picha ya mtoto chotara wa Kichina na Kitanzania, iliyosababisha mama yake kulalamika.
 
Mila na desturi zinasemaje?

Moja ya maswali hayo ni kama kazi hiyo inafuata mila na desturi za Kitanzania.

“Kinachofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kinakwenda kinyume na mila na desturi za Mtanzania kwa sababu masuala yanayohusu mzozo wa kifamilia na ndoa hufuata ngazi maalumu,” alisema Mwanaharakati wa haki za binadamu na masuala ya jinsia, Gemma Akilimali.
 
Mara zote kunapotokea mvutano unahusisha wanandoa kutoelewana au utata kuhusu mimba, watu wa kwanza wanaopaswa kutatua tatizo hilo ni familia na inapoonekana suala hilo linashindikana, jamii ya eneo hilo.”
 
Kisheria ni sahihi?

Pia suala jingine ni kuhusu sheria.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, mkurugenzi wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Tike Mwambikile alisema kitendo cha wanawake na watoto kupigwa picha na kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii si sawa.
 
Kuna mgongano wa kitaasisi?

Kuhusu baadhi ya mashauri kuwahi kuwasilishwa kwenye vyombo husika na hivyo kuwepo uwezekano wa maamuzi kugongana, Akilimali alisema si jambo la busara mkuu wa mkoa kuwakusanya watu sehemu moja na kuanza kusikiliza shida zao na iwapo ataendelea kufanya hivyo atakuwa amezipuuza taasisi nyingine, hivyo kuibua mvutano.
 
Mwantum Mgonja, ambaye ni miongoni mwa wanasheria wanaosikiliza malalamiko hayo, alisema wengi waliofika walianzia ustawi wa jamii na baadhi walifikisha masuala yao mahakamani.
 
Kampeni kutoa suluhisho la kudumu?

Baadhi wanaona jitihada hizo za RC zinaweza zisitoe suluhisho lenye ufanisi na mkurugenzi wa Chama cha Wajane (Tawia), Rose Serwati anaona kampeni hiyo inaweza ikachangia kuvunja ndoa za watu na kuweka uadui kati ya baba, mama na mtoto.
 
Lakini mhadhari msaidizi, Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Abigael Kiwelu alimshauri Makonda kutumia fursa hiyo kuelimisha wanawake hao ili wafikishe matatizo yao kwa maofisa ustawi wa jamii walioko kwenye kila kata.
 
Nini kitafanyika kwa wasioitikia wito

Wakati Makonda akitoa kauli kwamba wasioitikia wito kwenda kusikiliza malalamiko dhidi yao watatangazwa, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema Sheria ya Kanuni za Adhabu sura ya 16 kifungu cha 166 inawataka wazazi kulea na kutunza watoto wao.
 
Alisema mzazi anayekwepa kumlea mtoto au kumtunza hali ana uwezo, wa kumuhudumia atakuwa ametenda kosa la jinai.

Alisema Sheria ya Haki ya Mtoto ya mwaka 2009 inawahimiza wazazi na walezi kulea watoto wao na kutimiza majukumu yao yote.
 
Uhakiki wa madai yanayotolewa ukoje?

Katika kinachooneka kutaka uhakika wa madai dhidi ya wabunge wanaotuhumiwa kutelekeza watoto, Spika wa Bunge, Job Ndugai juzi aliwataka wazazi wenye malalamiko hayo waende kwake wakiwa na matokeo ya kipimo cha DNA.

Ndugai alisema inabidi ufanyike utaratibu ili kujua namna gani ya kushughulikia suala hilo.
 
Uhakiki wa madai yanayotolewa ukoje?

Katika kinachooneka kutaka uhakika wa madai dhidi ya wabunge wanaotuhumiwa kutelekeza watoto, Spika wa Bunge, Job Ndugai juzi aliwataka wazazi wenye malalamiko hayo waende kwake wakiwa na matokeo ya kipimo cha DNA.

Ndugai alisema inabidi ufanyike utaratibu ili kujua namna gani ya kushughulikia suala hilo.
 
Kuna ajenda ya siri?

Hata kabla ya kuanza kusikiliza mashauri hayo, tayari watu kadhaa walishatuhumu kuwa huenda mpango huo una ajenda ya siri na tayari baadhi ya wanasiasa wamesema bayana kuwa kuna njama za kuwachafua.
 
Tuhuma kama hizo ziliibuka pia wakati wa kampeni ya kusaka watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya iliyotaja pia wanasiasa na viongozi wa kidini.

Maswali mengine ni pamoja na kama kampeni hiyo itatoa fursa sawa ya kusikilizwa kati ya wanaume na wanawake na kama haki za kibinadamu zitafuatwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…