Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na sasa taarifa ya Ligi Kuu England ilitoa taarifa yake iliyosomeka: “Harry Kane amepewa lile bao la pili la Tottenham Hotspur dhidi ya Stoke City kwenye ushindi wao wa 2-1 Jumamosi iliyopita baada ya klabu na mchezaji kukataa rufaa Kamati ya Utambuzi wa Mabao ya Ligi Kuu England
 
Bao hilo mwanzoni alipewa Eriksen kwenye siku ile ya mechi, lakini baada ya taarifa za mchezaji na kutazamwa upya kwa picha za video, kamati ya watu watatu ilikubaliana mpira ulimgusa Kane kabla ya kutinga wavuni, hivyo bao hilo ni lake. Kane sasa atakuwa na mabao 25 Ligi Kuu England msimu huu wa 2017/18.”
 
Jambo hilo limemshtua Salah na kuamua kutumia ukurasa wake wa Twitter kuandika ujumbe huu: “Woooooow really?” akionekana kushangazwa na uamuzi huo. Fowadi huyo wa Liverpool amefunga mabao 29 kwenye Ligi Kuu England na ndiye kinara wa mabao. Mastaa kibao wa Liverpool na wanasoka wengine walionekana kubonyeza kitufe cha ‘like’ kuhusiana na komenti hiyo ya Salah kwenye Twitter.
 
PICHA ya beki wa kati wa Juventus, Giorgio Chiellini imenaswa na kuonyesha kuna kitu kinaitwa kupanga matokeo kilihusika kwenye mechi ya timu yake dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Bernabeu juzi Jumatano.

Juve ilitupwa nje ya michuano hiyo baada ya mkwaju wa penalti ya dakika za mwisho wa Cristiano Ronaldo, lakini picha ya Chiellioni akionyesha vidole vyake kama vile kuna pesa inatoka kupewa mwamuzi Michael Oliver akiituhumu Real Madrid baada ya uamuzi wa kupigwa kwa penalti hiyo iliyofanya mechi hiyo isiingie dakika za nyongeza baada ya Juventus kuchomoa bao zote tatu ilizokuwa imefungwa kwenye mechi ya awali.
 
Penalti hiyo ilitokana na beki wa Juventus, Mehdi Benatia kumwangusha Lucas Vazquez ndani ya boksi. Vurugu zikatokea na matokeo yake kipa Gianluigi Buffon akatolewa kwa kadi nyekundu.

Chiellini aliendelea kupinga matokeo hayo na kudai marefa wanaongoza kwa kuipendelea Real Madrid.

“Huu ni uporaji mkubwa niliowahi kuushuhudia katika maisha yangu ya soka,” alisema.
 
Weseeeeeee
Jamaniiii...

Hili neno tulikuwa tunalitumia JKT enzi hizo. Wanakuja watoto wa kishua kutoka Dar walaiinii wamefungasha misambwanda wanapewa vile vibukta vya kijani haviwaenei wakikimbia pwata pwata wanavishikilia basi sisi tunakoleza moto "Wese hiloo linakaribia kudondoka". We acha tu shemu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…