Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Afrika Kusini. Rais Cyril Ramaphosa pamoja na watangulizi wake Jacob Zuma na Thabo Mbeki walikuwa miongoni mwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mazishi ya mpigania uhuru, Winnie Madikizela Mandela yaliyofanyika kitaifa Jumamosi katika Uwanja wa Orlando, Soweto.

Mwili wa Winnie Mandela ulitarajiwa kupelekwa kwa maziko kwenye makaburi yaliyopo kitongoji cha Fourway umbali wa kilomita 40 Kaskazini mwa Soweto.
 
Waombolezaji waliimba sifa za Winnie wakati jeneza lenye mwili wa mwanamama huyo shujaa lilipokuwa likiingizwa kwenye uwanja huo umbali wa chini ya kilomita mbili kutoka nyumbani kwake.

Jeneza lake lilifunikwa kwa bendera ya Afrika Kusini na baada ya kuingizwa liliwekwa katikati ya uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 37,500 wote wakiwa wamekaa.
 
Waombolezaji walikuwa wamevaa mavazi ya rangi za chama tawala cha African National Congress (ANC), na za chama cha upinzani chenye siasa kali cha Economic Freedom Fighters (EFF), huku wakiimba “hakuna, hakuna kama Winnie”, wimbo maarufu kutoka enzi za harakati za ukombozi.

Mazishi hayo yamehitimisha siku 10 za maombolezo ya kitaifa kipindi ambacho maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walitoa heshima zao kwa “Mama wa Taifa” nyumbani kwake Soweto na kwingineko.
 
Winnie Mandela, aliyefariki dunia katika hospitali jijini Johannesburg akiwa na umri wa miaka 81, Aprili 2 baada ya kuugua muda mrefu, amepongezwa kwa kusaidia kuweka hai ndoto ya Nelson Mandela ya Afrika Kusini kuwa nchi isiyo ya ubaguzi wa rangi wakati yeye akiwa gerezani kwa miaka 27.

“Alikuwa mmoja wa viongozi jasiri katika chama cha ANC,” alisema mwombolezaji Brian Magqaza, 53. “Alipambana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Nenda Mama yetu nenda.”
 
Mfuasi wa EFF Mufunwa Muhadi, 31, alisema “Mama alipigania uhuru wetu. Ni muhimu sana kumpa heshima na tundeleze mapambano”.

Rais Cyril Ramaphosa, aliyeingia madarakani miezi miwili iliyopita, aliongoza waombolezaji katika misa iliyofanyika kwenye uwanja huo wa Orlando.
 
Marais wa zamani Jacob Zuma na Thabo Mbeki pia walishiriki. Lakini waombolezaji bila kujali huzuni zao walimzomea Zuma alipotangazwa kutambua uwepo wake.

Watu kadhaa mashuhuri kutoka nje walihudhuria wakiwemo viongozi wa Namibia, Swaziland na Jamhuri ya Congo, pamoja na mwanaharakati wa haki za binadamu Jesse Jackson wa Marekani. “Huyu ni mama halisi wa Afrika Kusini,” Jackson aliwaambia wanahabari.
 
Wakati wa ujenzi joketi alikua anawasimamia mafundi na maelekezo kibao ujenzi umeisha taishi mwanamke mwingine aiseeee
Hiyo nyumba ya tabata ndo ile wanasema jokate alikuwa anasimamia ujenzi??
[emoji23][emoji23]nacheka ka mazuri vile
Maisha haya basi tu
Huyo binti kikwunyilo chake hakinati? Kwanini kila mwanaume anafika na kuondoka?
Nakaonaga kapole katoto ka kingoni kale jamaniii!!!
 
Kutajwa kwa marais wawili wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na Jacob Zuma, kumeibua kelele za kuzomea zilizotoka kwa waombolezaji waliojitokeza kumuaga mwanaharakati Winnie Mandela leo.

Mwanamapinduzi huyo wa Afrika Kuisni, Winnie Mandela ambaye pia ni mke wa zamani wa Nelson Mandela, leo anaagwa katika uwanja wa Orlando. Alifariki Aprili 2 mwaka huu.
 
Kutajwa kwa marais wawili wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na Jacob Zuma, kumeibua kelele za kuzomea zilizotoka kwa waombolezaji waliojitokeza kumuaga mwanaharakati Winnie Mandela leo.

Mwanamapinduzi huyo wa Afrika Kuisni, Winnie Mandela ambaye pia ni mke wa zamani wa Nelson Mandela, leo anaagwa katika uwanja wa Orlando. Alifariki Aprili 2 mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…