Baada ya Ali Kiba kuoa, anayefuata ni dada yake Zabibu Kiba.
Zabibu anatarajia kufunga ndoa na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdi Banda.
Banda ambaye kwa sasa anaichezea Baroka FC ya Afrika Kusini, jana Ijumaa ilikuwa siku yake ya kuzaliwa, amethibitisha nia yake ya kumuoa Zabibu, ambaye ni dada wa Ali Kiba.