Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Barcelona 4-1 Arsenal, Aprili 2010

Sare ya 2-2 nyumbani kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya iliamsha matumaini kwa Arsenal kwamba wanaweza kuwasukuma nje ya michuano hiyo Barcelona. Na mambo yalizidi kuleta uhakika baada ya Bendtner kuifungia bao la kuonngoza kwenye mechi ya marudiano huko Nou Camp. Lakini, kumbe kulikuwa na Lionel Messi uwanjani, ambaye alizipindua ndoto za Arsenal kwa kufunga mabao manne peke yake kuifanya Barca kushinda 4-1 kwenye mechi hiyo na hivyo kusonga hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 6-3.
 
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kipigo kingine kizito ni kila alichokumbana nacho San Siro, Februari 2012 kwenye hatua ya 16 bora, ambapo Arsenal ilichapwa 4-0. Mabao ya AC Milan yalifungwa na Kevin-Prince Boateng, Robinho mawili na Zlatan Ibrahimovic kwa penalti.
 
Man United 8-2 Arsenal, Agosti 2011

Kipigo kingine kizito kwenye Ligi Kuu England Arsenal inakumbana nacho kutoka kwa Manchester United. Katika mechi hiyo, Wayne Rooney alipiga hat-trick, Ashley Young akapiga mbili, kisha mabao mengine mpira uliwekwa wavuni na Danny Welbeck, Nani na Park Ji-sung
 
Arsenal wao walipata mabao yao ya kujifariji kupitia kwa Theo Walcott na Robin van Persie na baada ya mechi hiyo Wenger aliingia sokoni kufanya usajili kuboresha kikosi chake, lakini ndiyo hivyo imebaki kwenye rekodi kwamba kipigo kilikuwa kizito.
 
Liverpool 5-1 Arsenal, Februari 2014

Liverpool ilianzisha kipindi kibaya kabisa kwa Arsenal baada ya kuwashushia kipigo kizito huko Anfield. Katika mechi hiyo, katika dakika 20 tu za mwanzo, Arsenal tayari walikuwa wamepigwa Bao Nne, kupitia kwa Martin Skrtel, aliyepiga mbili, Raheem Sterling na Daniel Sturridge. Mwanzoni mwa kipindi cha pili, Sterling alifunga tena na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 5-0, lakini ya vijana hao wa Wenger kufunga bao lao la kujifariji kupitia penalti ya Mikel Arteta.
 
Chelsea 6-0 Arsenal, Machi 2014

Mwezi mmoja baada ya kutokea kuchapwa 5-1 na Liverpool, Arsenal walikwenda kukutana na kichapo kingine kizito huko Stamford Bridge, walipokwenda kukumbana na kipigo cha Bao Sita Bila. Hiyo ilikuwa mechi ya 1000 kwa Wenger tangu aanze kuinoa Arsenal na bahati mbaya alikumbana na mbaya wake kwenye ligi, Jose Mourinho, aliyekuwa Chelsea kwa wakati huo. Hadi dakika 17,
 
tayari Chelsea walikuwa mbele kwa mabao matatu, yaliyofungwa na Samuel Eto’o, Andre Schurrle na Eden Hazard. Arsenal walipomteza mapema tu beki Kieran Gibbs kwa kadi nyekundu, ambayo alistahili kuonyeshwa Alex Oxlade-Chamberlain kwa sababu ndiye aliyekuwa amedaka mpira makusudi uliokuwa unaelekea wavuni. Chelsea iliongeza mabao yake kupitia kwa Oscar, aliyefunga mara mbili na Mohamed Salah akahitimisha hesabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…