Alisema mlezi wa watoto shuleni alimpigia na kumweleza aachane na mtu huyo kwa kuwa ni tapeli.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala alisema suala hilo linapaswa kushughulikiwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema hawajapata taarifa za matukio kama hayo, lakini akaahidi kuanza kuyashughulikia.