Sioni kama namna gani mstari wa mbele wa Real Madrid wenye Cristiano Ronaldo na Karim Benzema utashindwa kuziona nyavu za Lloris Karius. Ni kama ambavyo sioni wale mapacha watatu; Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino, wakishindwa kuziona nyavu za Keylor Navas.