Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilienda hoteli ya MWANZO kupitia barabara ya KUTOKA. Njiani niliona MAMBO YA WALAWI akichukua HESABU ya KUMBUKUMBU LA TORATI wakati YOSHUA alikuwa anasubiri katika lango zuri kwaajili ya WAAMUZI kumuona RUTHU akimuita kwa sauti kuu "SAMWELI SAMWELI".
Kwa hatua WAFALME wa kwanza na wa pili wa MAMBO YA NYAKATI wa kwanza na wa pili walikuwa wanakuja kumtembelea EZRA, NEHEMIA na ESTA kwa tatizo la AYUBU ndugu yao.
Walianza kuimba ZABURI na kuwafundisha watoto MITHALI zihusuzo MHUBIRI na WIMBO ULIO BORA .
Tukio hili lilitokea kipindi ISAYA alipokuwa katika kipindi cha MAOMBELEZO ya YEREMIA pamoja na EZEKIELI na DANIELI rafiki zao.
Wakati huo AMOSI na OBADIA hawakuwepo.
Siku tatu baadaye HOSEA, YOELI na YONA walisafiri katika meli moja pamoja na MIKA na NAHUMU kwenda Yerusalemu. HABAKUKI alimtembelea SEFANIA aliye mtambulisha kwa HAGAI rafiki wa ZEKARIA binamu yake na MALAKI.
Baada tu ya kuachana na desturi za kale, MATHAYO, MARKO, LUKA na YOHANA wakajihusisha na MATENDO ya WARUMI waliokuwa wanaenenda kama kundi la WAKORINTHO wa kwanza kwasababu kundi la WAKORINTHO wa pili halikupatana na WAGALATIA. Wakati huo pia waligundua kuwa WAEFESO na WAFILIPI walikuwa jirani na WAKOLOSAI.
Na pendekezo la safari ya WATHESALONIKE wa kwanza lilifanyika, katika safari yao ya WATHESALONIKE wa pili walipaswa kwanza wamuone TIMOTHEO wa kwanza na wa pili ambao ni ndugu waliokuwa wameenda kwenye nyumba ya TITO kumfundisha FILEMONI mdogo wake namna ya kusoma na kuandika kama WAEBRANIA.
Kwa kusikia hili, YAKOBO alimuuliza PETRO mara mbili kumfafanulia namna YOHANA wa tatu walivyomfunulia YUDA UFUNUO wa safari hii.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…