Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hili ni zaidi ya suala la kutazama mpira tu, ni njia ya maisha.

“Ni suala la kujali mchezo huu unaovutia, dhidi ya imani tulizojiwekea. Soka ni kitu ambacho kinaingia katika miili yetu, katika kila chembechembe za damu.
 
Tuna wasiwasi, tunajali, tunatamani, lakini unapokuja hapa, kituo cha ndoto zetu, tunafahamu soka ina maana gani.”

“”Ningependa kumshukuru kila mtu klabuni, nitawakaribisha, nitawasukuma hawa wachezaji na wafanyakazi ambao walikuwa nyuma yangu, hili kundi la wachezaji hapa lina ubora sana. sio tu uwanjani bali hata nje ya uwanja. Tafadhali ipeni sapoti hii timu kwa sababu inastahili.
 
Ningependa kumaliza kwa sentensi moja tu, nitawakumbuka sana, asanteni wote kwa kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu, asanteni sana. kwaherini” alimaliza Wenger.
 
PEP Guardiola na jeshi lake la Manchester City wanaendeleza kula bata baada ya juzi Jumapili kukabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu England, lakini huko kwa mpinzani wake, Jose Mourinho hakuna kulala kabisa.
 
Mourinho na mabosi wa Man United wameanza kupambana kusaka dawa ya kumzima Guardiola, ambapo harakati za kuingia na kutoka sambamba na vikao zimeshika kasi pale Old Trafford. Msimu huu Mourinho amekuwa mnyonge mbele ya Guardiola ambaye kikosi chake kimeuwasha moto kwelikweli na kutangaza ubingwa mapema kwa tofauti ya pointi 13 huku akiwa amepoteza michezo miwili tu.
 
Katika michezo hiyo aliyopoteza Guardiola mmoja amechapwa na Liverpool kwa mabao 4-3 kisha akachapwa na Man United mabao 3-2, ambapo kama Man United ingepoteza mchezo huo basi City ingetangaza ubingwa wake mbele ya United tena ndani ya Old Trafford.
 
Hata hivyo, Mourinho aliwaonya wachezaji wake mapema kuwa jeshi lake haliwezi kugeuzwa daraja la mahasimu wao kutangazia ubingwa na jeshi la Guardiola likafa tena kibabe kwelikweli.
 
Hata hivyo, Mourinho aliwaonya wachezaji wake mapema kuwa jeshi lake haliwezi kugeuzwa daraja la mahasimu wao kutangazia ubingwa na jeshi la Guardiola likafa tena kibabe kwelikweli.
 
Lakini, ishu kubwa inayoendelea Old Trafford kwa sasa ni usajili wa mastaa wa nguvu barani Ulaya, ambapo Mourinho na Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Ed Woodward wamejifungia na kutengeneza orodha moja matata ya mastaa ambao watakwenda kuvaa jezi za United msimu ujao.
 
Jose anataka kujenga kikosi matata kitakachotoa ushindani mbele ya vigogo wengine barani Ulaya kama Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, PSG na Manchester City ambayo imekuwa ikiwasumbua tangu ilipoanza kunolewa na Guardiola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…