Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Orodha ya mastaa hao kama Mourinho atafanikiwa kuwanasa wote basi ni tishio kubwa kama tetemeko na kamwe usiombe ukakutana nayo uwanjani ni lazima bao za kutosha zitakuhusu.
 
Jina la kwanza kuchomoza kwenye orodha ya mastaa wapya ambao Mourinho anawataka kwa ajili ya kutengeneza jeshi lake la msimu ujao lipo la supastaa wa Brazil, Neymar ambaye mipango iliyopo ni kumfanya kuwa mshambuliaji wa kati atakayekuwa panga pangua kwenye kikosi cha kwanza.
 
Kwa muda mrefu sasa, Man United imekuwa ikihusishwa na Neymar, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji ghali duniani baada ya kununuliwa na matajiri wa Paris, PSG akitokea Barcelona ya Hispania.
 
Usajili wa Neymar ulikuwa gumzo kwelikweli, ambapo PSG ililipa Pauni 198 milioni tena keshi kwa Barcelona na katika msimu wa kwanza tu, Mrazili huyo ameiwezesha kushinda taji la Ufaransa kabla ya kuumia na sasa yupo nje akiuguza majeraha.
 
Hata hivyo, kama dili hilo la kumnasa Neymar litajibu basi Man United watalazimika kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu England bila huduma ya kiungo wake fundi, Paul Pogba.
 
Iko hivi. PSG imekuwa ikijaribu kutaka kumsajili Pogba kutoka Old Trafford na taarifa zinasema kwamba, Man United wanaweza kuwa tayari kumhusisha kwenye dili la Neymar ambako, watatakiwa kuilipa PSG dau la Pauni 200 milioni pamoja na Pogba.
 
Habari zinaeleza kuwa, kwa Mourinho kumuachia mchezaji hata awe staa mkubwa kiasi gani halijawahi kuwa tatizo kabisa kwani, pengo linaweza kuzibwa na mastaa watatu ambao wako tayari kutua Old Trafford wakati wowote.
 
Katika mastaa hao kuna kiungo wa nguvu wa Stoke City ambayo imeshuka daraja, Xherdan Shaqiri anayepatikana kwa dau la Pauni 12 milioni tu kwa mujibu wa mkataba wake.
 
Pia, yupo kiungo wa Kibrazil anayetoa huduma yake pale Chelsea, Willian ambaye yuko tayari kuungana na Mourinho pale Old Trafford.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…