Mtawanyiko wa nywele mwilini huwa kama wa kiume, pamoja na ndevu msichana huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi kwa wingi. Wengine pia huota nywele nyingi kwenye makalio na kuzunguka sehemu ya njia ya haja kubwa na hali hii ya msichana kuwa na nywele nyingi mwilini, hujulikana kama “hirsutism”.