Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
***************************************
"Kabla Ya Kunivika Sanda Chukua Soksi Yangu Moja Univishe".

Haya ni ma neno ya Baba alomuusia mwanae muda mchache kabla ya kuaga dunia.

Watakapo nikosha kabla ya kunivika sanda chukua soksi yangu yeyote ya zamani univishe katika mguu wangu wa kushoto”.

Baada ya muda baba aliaga dunia na vilio vikatawala.
Watu walijaa kuja kutoa pole familia na kuanza taratibu za mazishi. familia ilimteua mmoja wa maimamu awe kiongozi katika kuosha maiti na kutengeneza sanda.

Walipomaliza kuosha kijana alikumbuka wasia wa baba yake, akaenda kuchukua soksi ili aipeleke kabla sanda haijafungwa, akamwambia Imamu samahani baba aliusia avalishwe soksi moja kabla hajatiwa sandani baada ya kukoshwa..

Imam kwa mshtuko alimjibu kijana kwa upole kuwa haiwezekani japo wasia wa marehemu unahifadhiwa, huyu hapaswi kuvishwa chochote zaidi ya sanda, kijana machozi yakimmwagika aliendelea kuhimiza wasia wa baba yake na kukatokea mzozo, wanasema avalishwe wengine asivalishwe.

Imam akasema wamtafute Sheikh mtaalamu wa sheria za dini ili atoe maelekezo, Sheikh alitafutwa na kuletwa msibani akawatuliza vijana na kuwaeleza kuwa wasia wa marehemu huwa unafatwa lakini si kila mahala, Marehemu hawezi valishwa soksi kwa kuwa si sehemu ya sanda.

Kuna mzee jirani yao alisimama na kumfata Kijana wa marehemu, akamwambia Baba yako alinipa barua nikupe kabla ya mazishi, Kijana akaipokea huku anatetemeka akaifungua na barua yenyewe ilikua inasomeka hivi:

"Mwanagu umeshuhudia mzozo ulipotaka kukamilisha wasia wangu, hawakukuruhusu kunivisha japo soksi moja tu tena ya zamani, Nimekuachieni mali nyingi na sasa ni za kwenu tambueni kuwa siku mtakapoondoka duniani hamtavishwa hata soksi na wala hamtoondoka na mali yeyote zaidi ya sanda zenu, hivyo mcheni mola wenu na tumieni mali hizo katika njia inayomridhisha yeye_"

Hili ni somo kubwa sana, Tujitahidi kuwa wema na kujiondoa kwenye gereza la umimi, ubinafsi na tuishi na watu vizuri, Mali zetu sii kitu bali ubinadamu wetu ndio wenye thamani kuliko mali zenyewe.
 
A good msg
Sheikh Shimba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…