Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Serikali inafikiria kufuta sera ya sasa inayowabana wazazi kuzaa mtoto mmoja, ofisa mmoja katika ofisi ya uzazi wa mpango amesema akitaja sababu kuwa kukabiliana na ongezeko la wazee katika jamii na pengo la kijinsia.
Sheria tata, ambazo zilikuwa zikiwabana wanandoa wengi wa mijini kuwa mtoto mmoja na vijijini kuzaa wawili tu, zilianzishwa miaka ya 1970 katika juhudi za taifa hili kubwa kudhibiti ongezeko la watu waweze kuendana na raslimali zilizopo.
 
Lakini sasa naibu waziri katika Tume ya Taifa ya Idadi ya Watu na Mpango wa Uzazi Zhao Baige alisema maofisa wanapitia maelezo ya kina kuhusu athari za kimazingira, kijamii na nyinginezo katika kubadili sheria.
Alipoulizwa ikiwa wana mpango wa kufuta sera ya kuzaa mtoto mmoja Baige aliwaambia wanahabari jijini Beijing kwamba kuna "mchakato mkali" wa kiutafiti hivi sasa.
Baraza la Taifa, ambalo ni Baraza la Mawaziri limeamuru ufanyike utafiti kuhusu madhara ya kuondoa sera hiyo iliyodumu karibu miongo minne ikitaka kuweka mabadiliko ya kitaifa, walisema watu walioomba wasitajwe majina wakati serikali inafanya majadiliano ili iweze kufikia uamuzi.
Uongozi unataka kupunguza pengo la wazee na kuondoa chanzo hicho kikubwa cha ukosoaji wa kimataifa, mtu mmoja alisema.
 
Mtu huyo alisema mapendekezo yanayojadiliwa kwa sasa yatakuwa mbadala wa sera ya kudhibiti idadi ya watu ambapo mmoja ameita kuwa ni “uhuru wa uzazi” kuwaruhusa watu kuamua idadi ya watoto wa kuzaa.
Mtu mwingine alisema uamuzi huo unaweza kutolewa mapema iwezekanavyo katika robo ya nne ya mwaka na kuongeza kuwa inawezekana tangazo rasmi linaweza kusogezwa hadi mwaka 2019.
 
Je, unapokuwa kwenye maongezi, wewe ni msikilizaji mzuri? Je, huwa inatokea unakutana na rafiki yako mchana na mnaongea lakini jioni unapokuwa peke yako unagundua kuwa hukumbuki hata alichosema.

Au inatokea kuwa uko katika gari lako ukiliendesha kuelekea mahali usipopajua bali ulielekezwa tu na hatimaye ukagundua kuwa umepotea. Kisha unaomba msaada njiani na kukuelekeza tena wakati ukiwa umekaribia unakokwenda.

Unaelekezwa na unaendelea hadi unafika njiapanda. Ajabu kabisa unasahau tena ulivyoelezwa kama upinde kulia au kushoto.
 
Ukweli ni kwamba wengi wetu huwa tunajiamini kama ni wasikilizaji wazuri lakini utafiti umethibitisha kuwa hii sio kweli. Tunahitaji kutambua mbinu zitakazoimarisha uwezo wetu wa kusikiliza na kuyazingatia kwa uthabiti yale tunayoelezwa.

Pamoja na mambo mengi yanayoweza kutujengea uwezo wetu wa kusikiliza tutajadili mambo manne yafuatayo. Mosi, ili uweze kusikiliza kwa makini wengine wanapoongea waachie nafasi ya kueleza hadi neno la mwisho. Epuka tabia iliyozoeleka kwa watu wengi ya kumkatikiza anayeongea.
 
Tena unapokuwa ukisikiliza usijishughulishe sana na kufikiria utakachomjibu hadi ukashindwa kuzingatia anachosema. Kuwa na uwezo wa kuweka uwiano mzuri kati ya kusikiliza anachosema mtu mwingine na kufikiria kile atakachomjibu au kusema atakapomaliza ni ustadi muhimu sana katika mazungumzo.

Hapana shaka kwa juhudi kila mtu anaweza kuijenga tabia hiyo hadi akaizoea. Pili, zingatia kuwa kila mtu huwa na mtindo wake wa kuongea, kuna wale wanaongea haraka na wale wanaoongea polepole.
 
Kadri utakavyomudu kupunguza kasi ya mazungumzo ndivyo kadri utakavyoweza kumuelewa vyema zaidi mtu unayeogea naye na aliyeko mbele yako.

Tumia ishara sahihi zinazostawisha maongezi kwani katika mazungumzo watu huvutiwa zaidi na ishara za mwili za muongeaji au msikilizaji kuliko hata maneno anayosema.
 
Hivyo, hata kama utajitahidi kusikiliza kwa dhati hutaonekana kama uko makini ikiwa utaonekana unatazama vitu vingine kama vile ukuta, dari au hata saa yako.

Kuna watu wenye tabia ya kupandisha na kushusha kichwa chini wanapokuwa wakisikiliza kuonyesha wanaafiki au wanaelewa kinachosema.

Kama ishara za mwili wako zitaonyesha kama hauko makini, mtu yeyote unayeongea naye hatajisika vizuri na pengine utamfanya hata asikueleze mawazo halisi yaliyo katika akili yake. Kila mara kumbuka unapokuwa katika mazungumzo kuna mtu anayefuatilia mwenendo wako na kuchunguza kila unachotenda.
 
Onyesha unafuatilia kile unachoelezwa katika maongezi huwa na maana maalumu iliyokusuduwa. Msikilizaji aliye makini ataonyesha jinsi anavyoathiriwa na kinachosema kwa kushangaa, kusikitika, kuhamasika na pengine hata kughadhibika.

Mtu anayesikiliza anapoonyesha anafuatilia ujumbe wa kuuliza maswali au kuongezea kwa kile kilichosemwa na mwenzake anaelewa vyema zaidi na kumhamasisha anayesimulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…