Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja huyu raia wa Hispania, mwenye umri wa miaka 46,aliisaidia klabu ya Psg, kutwaa mataji matatu katika msimu ulimalizika katikati ya mwezi huu na nafasi yake katika miamba hao wa Ufaransa imechukuliwa na Thomas Tuchel.
Kwa siku za karibuni kiungo wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ndio alitajwa angepewa jukumu la kupewa kazi ya umeneja ya kuwaongoza Arsenal baada ya miaka 22, ya kuongozwa na Arsene Wenger.
 
Wakati huo huo kiungo wa Arsenal Santi Cazorla anaondoka klabuni hapo msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake, Cazorla ameichezea timu yake jumla ya michezo 180 toka alipojiunga na klabu hiyo mwak 2012 akitokea Malaga.
 
CAKE TIPS / MASHARTI YA CAKE NA SIRI ZAKE :
Naomba niwafahamishe kwa ujuzi nilionao kuhusu cake.
Cake ni upishi mashuhuri duniani na ni upishi unaopendwa sana na watu mbali mbali duniani.
Cake ziko aina nyingi sana. Cake haina upishi wa namna moja. Mapishi ya cake ni mengi mno na ladha pia ziko nyingi mno.
Nawaletea siri za cake na ntawapa muongozo kwa njia nazojua.
 
1. Ondoa shaka kama huna maziwa eti huwezi kupika cake!!! Laa hasha!!! Maziwa ni hiari. Kama huna maziwa tumia maji ya vuguvugu na unapika cake bila ya tatizo. Haswa hizi cake za kawaida za vanilla na chocolate kama maziwa yamekosekana maji yanatumika na cake inaiva na kua nzuri tu. Ila pia kuna jambo la kuzingatia hapa... kama nilivyosema awali mapishi ya cake yako mengi na tofauti tofauti. Kuna cake zingine upishi wake unahitaji maziwa.. kuna cake zingine upishi wake unahitaji mtindi... kuna cake zingine upishi wake unahitaji siagi. Inategemea na upishi. Ila kama ni cake za kawaida sio lazima kuweka maziwa hata maji yanafaa.
 
2. Siagi pia inatatiza watu wengi. Ukiona upishi wa cake unahitaji siagi badala ya mafuta usipate tabu. BLUE BAND,PRESTIGE, KCC,KERI GOLD. Hizi ni siagi unaweza kutumia kwa kupikia cake. Na pia kuna cake zinapikwa mafuta. Kama umekosa siagi badala yake tumia mafuta..
 
5. sio cake zote zinapikwa na mayai... kuna cake ambazo haziwekwi mayai. Kuna cake ambazo haziwekwi baking powder. Kuna cake ambazo haziwekwi baking soda. Kuna cake za matunda makavu. Kuna cake za matunda fresh. Kuna cake za aina nyingi. Na kila upishi wa cake una mahitaji yake. Ukifata mahitaji na vipimo sahihi basi umeshafanikisha.
 
3. Unapoweka cake ndani ya oven au hata kama utapika katika jiko la mkaa... usipende kufungua mara kwa mara.. hewa inapotoka nje.. cake hubonyea katikati na pia kutoka mbichi kwa ndani. Unapoweka cake ndani ya oven au katika jiko mkaa... kua mstahamilivu na fungua kwa nadra sana. Na unapofungua fungua kidogo sio unafungua yote hewa ikitoka matokeo ya cake yanakua sio mazuri.
 
7. Sio cake zote lazima ziwe Zina baking powder. La hasha!!!! Mapishi ya cake yako mengi duniani na tofauti tofauti.. ukiona katika VIFAA vya cake hakuna baking powder usishtuke. Cake zingine hutumia bicarbonate of soda. Na cake zingine hazina ngano na cake zingine hazina mayai.
 
11. Pia wengi hulalamika kua cake zinapasuka kwa juu... cake zinapasuka kwa juu kwasababu ya chombo kua kidogo na kwahiyo Kubana nafasi ya cake pale inapoumuka na kufanya cake kupasuka kwa juu.. hakikisha unakadiria upana wa chombo na mchanganyiko wa cake. Hapo utapata cake inatoka vizuri kabisa juu bila ya kupasuka.
NI MUHIMU KUFATA MASHARTI YA KUPIKA CAKE KWAJILI YA KUPATA CAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…