Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar ameungana na wachezaji wenzake kwa mara nyingine jana kwa ajili ya maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia Juni.
Kikosi cha Brazil kiliwasili Jumatatu Granja Comary tayari kwa ajili ya mazoezi ikiwa ni safari yao ya maandalizi kuelekea Kombe la Dunia.
Mchezaji Neymar aliwasili ilipoweka kambi timu hiyo kwa kutumia helkopta akiwa ameambatana na wachezaji wenzake Douglas Costa, Renato Augusto na Thiago Silva.
Pia wachezaji hao wataungana na wachezaji wenzao kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya afya zao.