Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanakemia wa Hungary George de Havesy aliyeyusha tuzo za Nobel za wanafizikia wa Kijerumani Max von Laue na James Franck, ili kuzuia utawala wa Kinazi kuzitaifisha. Hata hivyo tuzo hizo za dhahabu ziliundwa tena upya baada ya vita.
 
Huko dubai kuna ATM kwa ajili ya kutolea vitofali vya dhahabu. Je wajua kuwa utajiri huweza kuhifadhiwa kwa vipande au vitofali vya dhahabu? Basi huko dubai matajiri wanaweza kutoa vipande hivi kwenye ATM kama watoavyo pesa.
 
Mwanasiasa wa Kirumi Gaius gracchus, kichwa chake kilihitajika kwa malipo ya dhahabu sawa na uzito wake. Hivyo atakayemuua na kupeleka kichwa chake angepewa dhahabu sawa na uzito wa kichwa hicho. Hata hivyo dhahabu hii haikulipwa kwa mtekaji kwa sababu alikijaza kichwa hicho madini ya risasi ili kiwe kizito zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…